Posts

    UMUHIMU WA KUJIJENGEA UWEZO ILI KULIBEBA KUSUDI LA MUNGU   KATIKA MAISHA YAKO. (CAPACITY BULDING).   NA MWL. MUSA FESTO   MAANDIKO YA MSINGI. "Lakini, kueni katika neema , na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele"(2Petro 3:18).     " Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote"( Wagalatia 4:1)   MISINGI YA UUMBAJI.   Mungu alipokuwa anamuumba mwandamu na kumleta duniani kwa ajili ya kusudi lake kuna kiwango maalumu cha "kiutumishi"(kusudi na mapenzi makamilifu ya Mungu) ambacho Mungu alimpangia kila mmoja ili kwa kiwango hicho mwanadamu alitumikie kusudi la Mungu katika nyanja mbalimbali za kielimu,kiuongozi,kisiasa,kihuduma,kifamilia,kazi.n.k.     "Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo"(Waefeso 2:10)....