SOMO: HUDUMA
“Tena
pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye Yule”.
1
Wakorintho 12 :5
HUDUMA NI NINI?
Huduma
ni kazi ambayo mtu hupewa/kapewa na Mungu aifanye kwa uongozi wa Roho Mtakatifu
kwa ajili ya kuwafanya watu wamjue Mungu na kudumu katika maisha matakatifu
ili wawe na uzima wa milele.
Huduma
ni kazi apewayo mtu na Roho wa Mungu ili apeleke ujumbe wa Mungu kwa watu.
Mfano
1. Utume
2. Unabii 3.
Uchungaji 4. Uinjilisti 5. Ualimu
“Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni
yeye Yule”. 1 Wakorintho 12 :5
Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, *wa kwanza
mitume* , wa *pili manabii* , *wa tatu waalimu,* kisha miujiza, kisha karama za
kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha. Je! *Wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni
waalimu?* Wote wanatenda miujiza? 1
Wakorintho 12:28 – 29
Huduma ni kazi ya Kiroho
Naye
alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti
na wengine kuwa wachungaji na waalimu; Waefeso
4:11
Huduma ni wito ambao mtu huitwa na Mungu hata
kabla ya kuzaliwa kwake.
Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla
hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. Yeremia 1:5. Mungu alimjua Yeremia tangu tumboni mwa mamaye. Pia alimjua Yohana tangu tumboni mwa mamaye.
Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria,
maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina
lake utamwita Yohana. Nawe utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi
watakufurahia kuzaliwa kwake. Kwa
sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa
Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye. Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao. Naye
atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo
ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea
Bwana tayari watu waliotengenezwa. Luka 1:13 - 17
KARAMA
ZA HUDUMA TANO (Efeso. 4:11)
Katika kitabu cha
Waefeso 4:11 Mtume Paulo ameweka wazi huduma katika nafasi Tano na lengo za
huduma hizi katika kanisa ni KUWAKAMILISHA WATAKATIFU HATA MWILI WA KRISTO
UPATE KUJENGWA.
Mwili wa Kristo ni
KANISA.
1.
Huduma ya Utume/Mtume
a)
Mtume (Gk. Apostolos = aliyetumwa /
pelekwa.
Neno hili Lilitumika
kuelezea au kuwakilisha;
i. Balozi
ii. Kikundi cha merikebu
kilichopelekwa ili kuanzisha koloni jipya
iii. Nahodha anayeamuru
merikebu hizo.
iv. Koloni
lililoanzishwa na nahodha.
b)
Mtume ni mtu wa umisheni, Mwenye
kumuwakilisha na kuyafanya mapenzi yake aliyempeleka/aliyemtuma. Ni asemaye na
kutenda kwa niaba ya mwingine.
Yesu Kristo ndiye
mwanzilishi wa Utume kwani alipelekwa na Baba yaani Mungu kuyafanya mapenzi ya
Baba/ Mungu. YESU kama Mtume na Mitume Aliowaweka (Yoh. 6:38, 12:49 - 50)
Yesu Kristo aliwaweka
Mitume kwa kusudi au lengo
·
Wawe mabalozi/ Mitume –kumuwakilisha
ulimwenguni
·
Waanzishe koloni jipya - yaani Kanisa, Koloni la kifalme, lenye mamlaka
ya Ufalme wa Mungu nyuma yake. Na hapo kwanza kanisa la kwanza liliitwa Kanisa
la Mitume.
·
Ili kupata Kanisa ambalo mapenzi ya
Mungu yanatimizwa ulimwenguni kama vile mbinguni. Yoh. 20:21, Mt.10:40; 16:18, Efe.2:20
Aina
/Viwango Vya Mitume Katika Agano Jipya
Vipo viwango vya aina
nne vya huduma ya Utume, kati yake viwili havitendi kazi tena kwa hivi sasa. Viwango
hivyo ni:-
1.
YESU KRISTO – Mtume Mkuu aliyekuwako na
aliyeko. (Ebr.3:1, Yoh.3:16, 20-21; Yoh. 4:34, 5:19, 30; 6:38; 8:28 ,29, 42; 12: 44 - 45)
2.
Mitume Kumi na wawili wa Mwana Kondoo (Ufu.21:14,
Mt.19:28)
Hawa walichagulia na
Yesu Kristo mwenyewe baada ya mkesha wa usiku kucha wa maombi mazito. Hawa wana
nafasi maalumu mbinguni na milele, majina yao yameandikwa katika misingi kumi
na mbili ya mji Mtakatifu – Yerusalemu.
Ni alama ya mwanzo wa
kizazi kipya, na mwisho wa zama za unabii.
Katika agano jipya ni Mitume
waliohusika na uandishi wa maandiko Matakatifu
Katika agano la kale ni
Manabii waliohusika na uandishi wa maandiko matakatifu.
3.
Mitume waliotokea baada ya kupaa kwa
Bwana (Efe.4:10-11)
Mitume hawa watatenda
kazi hadi kanisa liufikie umoja wa imani na kumjua Mwana wa Mungu. (Efe.4:13)
Ni wamuhimu sana katika
mwili wa Kristo. Wasipokuwepo kanisa litaumia kutokana na kukosa uongozi wa
maeneo mengi muhimu. (1Kor 12: 26-28)
Mifano Ya Mitume Hawa
Katika Agano Jipya.
i. Androniko. Rum.16:7
ii. Yunia. Rum.16:7
iii. Tito. 2Kor.8:23
iv. Barnaba. Mdo.14:14
v. Yakobo. Gal:1:19
vi. Epafrodito.
Fil.2:25
vii. Timotheo.
1The.1:1; 2:6
viii. Silvano.
1The.1:1; 2:6
ix. Apolo. 1Kor 4:6, 9.
4.
Wale Wengine Sabini (Wenye Huduma ya/
Ifananayo Na Utume)
Siyo lazima waitwe Mitume,
bali huitenda / huitimiza huduma ya Kiutume.
Mfano; wale wengine
sabini ambao Bwana Yesu aliwatuma (Luk.10:1-17)
Leo
Je Mitume Wanahitajika?
Watu wengi leo hii
katika kanisa hawaamini kwamba wapo mitume kwa nyakati hizi (au hata Manabii) Wanazikubali karama nyingine kama ya uinjilisti,
uchungaji, na ualimu; sababu eti mara kanisa lilipoanzishwa katika karnee ya
kwanza, hatuhitaji tena mitume na manabii, lakini je, mawazo haya ni sahihi
kulingana na maandiko? (Efe.4:11-13).
Hapa
biblia imeweka wazi kwamba karama za huduma tano ni za kutenda kazi “hata
sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata
kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;”
Yaani, kanisa liufikie;
1. Umoja
wa imani
2. umoja
wa maarifa ya kumjua sana Mwana wa Mungu
3. Cheo
cha kimo cha utimilifu wa Kristo.
Kwa
kulipima kanisa leo hii, bado hatujafikia maeneo haya yote, kwa hiyo kanisa
linahitani karama ya huduma zote tano; ikiwemo ya huduma ya mitume.
Lakini je, leo hii wapo Mitume katika kanisa ?
BWANA
Yesu Kristo bado leo hii anawatuma aliowaita na kuwapa agizo katika nguvu za
Roho Mtakatifu na mamlaka, ili wafunge na kufungua, wahubiri injili, waponye
wagonjwa na kufufua wafu, katika nguvu za Kristo mfufuka; kuwafikia walio
gizani wangojeao kuiona nuru kuu ya Kristo YESU! Kumbuka! Jina “Mtume” Siyo la
lazima, kwa sababu uthibitisho wa huduma ya kitume unaonekana katika tunda
lizaliwalo kwa kazi ya Kiutume. (1Kor.9:1,2).
Sehemu Muhimu Ya Mafunzo Ya Mtume
1. Wito
dhahiri katika huduma hii.
2.
Kufunzwa vizuri maandiko.
3. Kuandaliwa
muda wa miaka kadhaa.
4.
Kujifunza chini ya huduma ya mitume wengine.
5.
Kutumiwa na Mungu kati ya huduma nyingine zilizopo katika huduma tano
zilizobaki.
6. Hatatumwa hadi maandalizi yake yamekamilika.
7. Kanisa linalompeleka, litamtambua na kumuwekea mikono kabla
ya kwenda.
Sifa Za Mtume
Viwango/sifa
za wazee zinatumika kwa viongozi wote katika ngazi za juu za mamlaka ya Kimungu
na kwa mtume pia. (1Tim.3:7, Tit.1:5-9)
Licha ya viwango hivi, zipo sifa maalumu au tabia maalumu ambazo kila mtume
anapaswa kuwa nazo, ambazo ni:-
1. Moyo wa
Mzazi. (Kor.4:15, Fil.2:22, Efe.6:4, 1The.2:6-8,11)
2. Mwenye
Saburi (2Kor.12:12)
3.
Mwaminifu (1Kor. 13:)
4. Asiwe
Mwenye Kujitukuza (1kor.4:9; 2kor.10:8, 1the.2:6)
5. Mwenye
Moyo Wa Kutumikia, Sio Kutumikiwa. (Efe.3:7; Fil.1:11; 1kor.4:9, 2kor.10:8;
1the.2:6)
6. Awe
Tayari Kuteseka (Mdo.20:17-24; 1kor.4:7-12; 11:18-30)
Huduma Ya
Mtume Kazi za mtume ni kama ifuatavyo:-
1.
Kuanzisha Makanisa na kuyaweka katika msingi sahihi. (1Kor.3:9-14; 9:12; 11:34;
Efe.2:2-4; Rum.1:11; Kol.2:5-7)
2. Kutoa
mafundisho na maandiko sahihi. (Mdo.2:42; 15:1-31)
3. Huduma
ya matendo ya miujiza. (Rum.15:18, 19; 2Kor.12:12)
4.
Kuliadibisha kanisa pale inaphitajika. (Mdo.5:1-11, 1Kor. 5:)
5. Kuweka
uongozi katika kanisa jipya. (Mdo.6:1-6; 14:23; Tito.1:5)
6.
Kuwafundisha na kuwafunza watendakazi wapya. (2Tim.2:2; Mdo.16:1-4; Fil.2:19-20;
Kol.4:7-12)
7.
Maangalizi ya makanisa aliyo yaanzisha. (2Kor.11:28)
8.
Kutenda kazi na wazee wa kanisa, katika kuweka watendakazi wapya. (Rum.1:11;
1Tim.1:18; 4:14; 2Tim.1:6) – Kufunga na kuomba, Kuwekea mikono.
9. Kuwa mfano wa kama mzazi (baba au mama) katika familia ya Mungu. (1Kor.4:15;
1Kor.16:12, 1Pet.5:2)
10.
Kuhusisha karama za huduma nyingine nne.
Mtume
anatakiwa kuwa:-
Mwinjilisti-
Ili kuwafanya waamini wapya.
Mwalimu-
Ili kufundisha/kuelekeza katika mafundisho ya kweli.
Nabii -
Ili kuleta mwelekeo na masahihisho kwa nguvu na mamlaka ya kimungu.
Mchungaji
- Ili kuangalia kazi ya watendakazi wapya na makanisa. Huduma ya mtume ni ya
pekee na ni mbali na huduma nyingine nne zilivyo; Mfano:-
Ni kama mkono wa binadamu, wenye vidole vine na dole gumba; Mtume ni kama dole
gumba, ambalo huvigusa kirahisi vidole vingine vyote vinne, ila sio rahisi kwa
kidole kingine chochote kuvigusa vidole vingine vinne, isipokuwa huweza kugusa
dole gumba tu; -hiyo ina maana kuwa waamini wote wamepewa agizo kuu, umisheni!
Wito wa Mtume. Mtume huitwa na Mungu. Ni Mungu aamuaye wapi,
lini, na ni jinsi gani mtume atahudumu. Kwa ajili hiyo, mtu hatakiwi kirahisi
rahisi tu kujiita mwenyewe kwamba yeye ni mtume (au nabii, muinjilisti,
mchungaji, au mwalimu) WITO WA MTUME UTAJULIKANAJE? Nani atamtambua na kuithibitisha
huduma yake? Njia za kufahamika na
kutambulika.
1.
Kujifahamu na kuwa na hakika kwa habari ya wito wake.
2.
Viongozi wa kanisani kwake watamtambua kwa kazi zake.
3. Kazi
zake zitamjulisha.
4. Watu wa
kanisa la nyumbani/mahali nao watamtambua. Hii haimaanishi kwamba atajulikana
au kupokelewa kama mtume na kanisa kiulimwengu. (1Kor.9:1-3)
2. Karama Ya Huduma Ya Nabii.
Nabii:
Kiebrania = Nabi; Msemaji wa Mwingine, Mjumbe; Hozeh, Roeh = Kuona, Mwonaji.
Mjumbe, Mtu Wa Mungu. UNABII Ni Ujumbe Wa Nabii. Maono, Mzigo, Utabiri Au Neno
La BWANA. Kazi Za Nabii
1. Kusema
Ujumbe toka kwa Mungu. (Ebr.1:1)
2.
Utabiri wenye kufunua mawazo ya Mungu, kwa
a.
Utabiri wa matukio yajayo, ambayo Mungu tu huyajua (Mdo.21:10-14)
b. Kuweka
wazi mawazo, nia, na makusudio ya moyo wa mwanadamu (Mdo.5:3)
Yote ni
kwa uongozi wa Roho Mtakatifu na sawa na unabii wa kibiblia.
Mara nyingine mahubiri huweza kuwa ya kiunabii pale ukweli ambao haukufikiriwa
kwanza au utendaji unaletwa mara na Roho Mtakatifu kupitia chombo kiteule kama
vile Mchungaji, Mwalimu, au mzee ambaye hana karama ya huduma ya Nabii. Nabii
atauweka wazi na huutangaza moyo au nia ya Mungu kwa watu na atafunua moyo na
mawazo ya watu mbele za Mungu wakati anapohudumu.
Viwango Vya (Aina Za) Unabii.
1. Unabii Wa Kimaandiko (2petr. 1:19-20) Ni
unabii wa halli ya juu sana.
Unatolewa kwa uvuvio wa Mungu (2Tim.3:16) Hauna makosa Una mamlaka kamili / ya
mwisho. Hautolewi tena siku hizi za leo (Ufu.22:18-19). Biblia ni kamili ni
kiwango cha kupimia aina nyingine zote za unabii.
2. Huduma/Karama ya Unabii (1kor.2:10) Ni
mojawapo kati ya karama tisa zitolewazo na Roho Mtakatifu. Mwamini yeyote
huweza kutumiwa wakati fulani (Mdo.2:18)
Ni kwa ajili ya kuujenga, kuuhamasisha, na kuufariji mwili wa Kristo.
(1Kor.14:3)
Atumiwaye kwa karama hii, haina maana kwamba yeye ni Nabii! (Hes: 11:22, 1Kor
14:24,31)
3. Karama
Ya Huduma Ya Nabii Inahusiana na wito wa mtu.
Ni karama
ya huduma itolewayo na BWANA YESU kwa aliyeitwa kwenye wito wa huduma ya kiuongozi
katika kanisa. Kazi zake ni;
o
Kuthibitisha
o
Kuongoza / kuelekeza
o Kukemea
o
Kuhukumu / kuamua
o
Kuadibisha / kurekebisha
o Kuonya
o Ufunuo.
Asili Ya Huduma Ya Kiunabii. Mungu
mara zote aliiweka sauti ya kiunabii ulimwenguni. Alichagua kusema kupitia
viongozi wa kimungu hata kabla ya huduma ya nabii kutolewa.
o Habili (Luk.11:50-51) o Henoko (Yud.14) o Nuhu (Ebr.11:7, 2Petr.2:5)
o Abramu (Mwa.20:7) o Isaka (Zab. 105:9-15) o Yusufu (Mwa.50:24) o Musa (Kum.34:10) o Miriamu (Kut.7:10) o Haruni (Kut.7:1)
o Debora(Amu.7:1)
Mungu alimpa Musa mwongozo wa kuwapima Manabii wote watakao tokea baadaye.
Hes.12:6 Kum.18:15-22 Isa.8:19-20 Luk.16:29. Huduma maalumu ya nabii ilitolewa
kwanza kwa Samweli (Mdo.3:24-25,
13:20, Ebr. 11:32)
Samweli alianzisha pia shule ya manabii. Alikuwa ni mwamuzi wa mwisho na wa
kwanza kwa wale walioitwa kwa ajili ya Karama ya Huduma ya Nabii. (2Fal.2:35) Aliuweka
mpangilio mpya wa kiunabii kwa watu. Walifundishwa katika neon Walikuwa makini
sana kwa sauti ya Roho Mtakatifu Walimwabudu Mungu katika Roho na kweli Kila
nabii alikuwa nasehemu katika urithi wa kiunabii Katika kila mfalme wa Israeli,
nabii aliinuliwa ili kumweka katika njia sahihi. Miaka 400 K.K. sauti ya unabii
ilikuwa kimya. Kisha ikaanza kusikika tena kwa kinywa cha Yohana Mbatizaji. Kipindi
cha Agano Jipya walikuwepo manabii katika Matendo ya Mitume, kama ifuatavyo:-
MANABII WA AGANO JIPYA i. Yuda na sila (Mdo.15:32) ii. Agabo (Mdo.22:10-13) iii. Anania (Mdo.22-15) iv.Katika Antiokia (Mdo.13:1) v. Katika Tiro (Mdo.21:3-4) vi. Katika Yerusalemu (Mdo.11:27) vii. Katika Korintho (1Kor.14:29).
Mungu
aliihuisha tena huduma iliyonyamaza kwa muda wa kipindi kirefu. Yesu Kristo –
Nabii Ambaye Ni Kielelezo. Aliitwa nabii wa Mungu (Kum.18:15, Mdo.3:22). Watu
wegi walimwona kuwa ni nabii. (Yoh.4:19; 16:14; 7:40; 9:17; Ebr. 1:1-2) Alisema
yale tu aliyoyasikia kwa Mungu na aliyoyaona toka kwa Mungu alitoa unabii wa
mambo yajayo Ni nabii mkuu. Kazi ya Huduma Ya Nabii
1. Huduma
ya nabii huwa tofauti kati ya nabii na nabii, hazifanani kabisa.
a. Majina
huonyesha hilo pia. i. Waonaji
(1Sam.9:9) ii. Wajumbe (2Nya.36:16)
iii. Watu wa Mungu (2Fal.12:22) iv. Watumishi wa Mungu (Amo.3:7, Zeka1:6)
b. Walipokea mafunuo yao kwa njia tofauti. i. Kwa kuona vitu katika Roho. (Mfano:
- Ezikieli, Danieli na Zekaria). ii. Kwa njia ya ndoto / njozi. Kupatwa na hali
ya usingizi, au kuhamishwa- kama vile roho kuondolewa katika mwili, kisha kuona
vitu katika ulimwenug wa kiroho.(Mfano:-Daniel, Paulo, Yohana)
iii. Kwa kusikia sauti. Kusikia vitu katika roho. (Mfano: - Mika, Isaya, na
wengineo)
c.
Waliwapa watu ujumbe wao kwa njia tofauti pia. i. Kwa kusema (Isa.21:6)
ii. Kuandika (Yer.30:2) iii. Kwa mifano ya kuigiza au hadithi za kweli.
(Eze.4:1-3; Mdo. 21:11) Hosea na Yoeli walitumia mifano na hadithi.
Huduma Ya
Nabii Katika Agano Jipya Itahusisha 1) Ufunuo kwa: -
a) Mtizamo wa ndani wa kimungu katika neon au nia ya Mungu.
b) Ulitumiwa na mituma na manabii katika kuandika Agano jipya (Efe.2:20, 3:4-5.
c) Mtizamo maalumu wa ndani katika maisha ya watu(Mdo.5:1-11; 1Kor.14:25)
2) Mtizamo maalumu wa ndani kwa matukio yajayo (Mdo.11:27-28, 21:10-14) Nabii
hawatawali viongozi au kanisa bali hutoa mwelekezo/mwongozo tu!
3) Kuhamasisha / kuchochea / kutia moyo. (Ezr. 5:1-2; 6:14; 1Kor.14:3-4; Efe.4:11-12)
4) Kuonya, kutahadharisha (Mdo.11:27-30; 21:8-11 –Ili wajiandae kwa busara kwa
yale yajayo.
5) Maono
kwa watu wa Mungu (Mit.29:18; Amo.3:7; Efe.3:5) –ili kutoa mwelekeo.
6) Kuanzisha
makanisa mapya. (Efe.2:20; 3:5; Mdo.15:32, 41; 13:1-3)
7) Kuhudumu na manabii wengine (na mitume) kama timu au kikundi. (Mith.11:14,
Mdo.11:14, Mdo.11:27-30, 1Kor. 14:29) - Ili kuleta uwiano na kuepushwa katika
makosa ya kibidamu. Maonyo Kuhusu Huduma Ya Nabii
1) Maonyo
ya Mungu kwa watu wake kuhusu ~ a) Kuipokea huduma ya nabii (Mt.10:41) i)
Kutowakataa manabii – Mt.13:57, Mk.6:4 1The.5:20)
ii)
Kanisa halitakua itakiwavyo kama manabii watakataliwa (Luk.11:48-51). b)
Kujihadhari na manabii wa uongo (Yer.5:30, 31; 14:13-18; 23:9-40; Eze.13:1-23,
Mt.7:15, 24:11, 24) Kuwapima kwa kupitia
(1) Neno
la Mungu (2) Roho Mtakatifu. (3) Viongozi wa kiroho. (Isa.8:20, 1The.5:20-21,
1Yoh.4:1)
2) Maonyo
ya Mungu kwa manabii wake. i) Wawe na kiasi (1Kor.14:32)
ii) Waruhusu huduma yao kupimwa. (1Kor.14:29) – Hakuna asiyekosea.
Njia Za Kuipima Karama Ya Huduma Ya Nabii. (1yoh.4:1)
a) Unabii
unakubaliana na neno la Mungu? (Isa. 8:20).
b) Umetolewa
kwa roho njema? (1Kor.13:2) c) Maneno ya Unabii yametimia? (Yer.23:13 – 16)
d)
Ushuhuda wa Roho Mtakatifu unaendana na unabii? (2Petr.1:21)
e)
Viongozi wa kiroro wengine wanaukubali? (2Kor.13:1)
f) Maneno
ya unabii yanawaongoza watu kwa BWANA au mbali naye. (Kumb.13:1-4).
3. Karama Ya Huduma Ya Mwinjilisti.
(Mshuhudiaji/Mhubiri)
MAANA
Evanggelizo = kuhubiri, kutangaza, kutamka habari njema -
kushuhudia.
Evanggelion = Injili au habari njema
na ujumbe wa furaha.
Evanggelistes = Mhubiri au mjumbe wa
habari njema.
KRISTO YESU – KIELELEZO CHA MWINJILISTI
Luk. 4:43, 4:18-19, Isa.61:1-2,
Agizo alilotoa katika Mk.16:15
Huduma Ya Mwinjilisti / Mshuhudiaji / Mhubiri
Katika Matendo ya Mitume sura ya .21:8, kuna Mwinjilisti wa kanisa la kwanza aliyekuwa akiitwa Filipo.
Huyo alikuwa na huduma ya Uinjilisti.
Mambo
manne ya kujifunza kutoka kwa Filipo kuhusu uinjilisti;-
1.
Maandalizi Ya Mwinjilisti (Mdo.6:1-6)
a. Hutoka
katika kanisa la mahali pamoja
b. Mtu wa
tabia njema na mwenendo mzuri kiroho
c. Aliyejazwa
Roho Mtakatifu na hekima.
d. Aliye
na moyo wa kitumishi wa upendo
e. Aliye
jithibitisha kwanza kuwa ni shemasi
f. Aliye
jinyenyekesha katika mamlaka ya kimungu kupitia uongozi wa kanisa la mahali
pamoja.
g.
Aliyeungojea wakati wa Mungu. (Mdo.8:1-5)
2.
Huduma ya Hadharani (Pamoja) Ya Mwijilisti Filipo ni mfano:(Mdo.8:5-25)
a. Katika mahubiri yake
i. Kristo Yesu ndiye
kiini. (Mdo. 8:5-12) kwa sababu
ndiye asili ya Injili
ii. Kuliambatana na ishara
na maajabu ya Mungu. (Mdo.8:6-7)
b. Aliwabatiza katika maji
mengi waamini wapya kama ishara ya imani (Mdo.8:12)
c. Aliwatuma kwa Petro na
Yohana aliyewaongoza katika Ubatizo wa Roho Mtakatifu.
d.Waamini wapya waliwekwa
katika kanisa la mahali pamoja (Mdo.9:31)
e. Hakwenda tu kuhubiri bali mpaka pale BWANA alipompa maelekezo. (Mdo.8:26), aliitii sauti ya Mungu.
f. Alikuwa na “uinjilisti
wenye shabaha/malengo” – yaani, wenye makusudio ya kuwapata waamini wapya. (Mdo.8:14-17)
3.
Huduma Ya Binafsi (Ya Kumhubiria Mtu Mmoja Mmoja – Isiyo Ya
Hadharani) Mdo.8:26-40) Inahitaji:-
a. Kuwa makini kuisikiliza
sauti ya Roho Mtakatifu na kutii.(Mdo.
8:26 - 40)
b. Kuwa na ufahamu mzuri
wa neno la Mungu. (Mdo. 8:35)
c. Kuwa na uwezo wa
kuielezea vizuri njia ya Mungu ya wokovu kupitia Kristo Yesu. (Mdo. 8:35)
d. Kuhudumu kwa yule
ambaye moyo wake uliandaliwa tayari na Mungu. (Mdo. 8:30)
e. Kuongoza kumkiri Yesu
Kristo kama BWANA na Mwokozi (sala ya toba) yaani kutoa nafasi ya uamuzi wa mtu
kumpokea Mwokozi Yesu. (Mdo. 8:37)
f. Kutilia muhuri uamuzi
wa waamini wapya kwa Kristo kwa ubatizo wa maji mengi. (Mdo. 8:38)
4.
Wajibu Wa Mwinjilisti Katika Mwili Wa Kristo. (Mdo.4:11-13)
a. Kusafiri na kuhubiri injili sehemu ambako hawajasikia habari za wokovu.
b. Kuwafundisha na kuwazoeza wengine
katika kanisa la mahali jinsi ya kufanya uinjilisti (Kushuhudia) kwa
waliopotea.
4. Karama Ya Huduma Ya Mchungaji
Waamini
huitwa kundi la kondoo wa Mungu. (Isa.40:11,
Yer.13:17, Mt. 26:31, Yoh.21:15, 1Petr.5:2).
Kondoo
wanazo tabia nyingi zinazotukumbusha kwa habari ya wakristo wapya/waongofu
wapya katika kujifunza kukua katika BWANA.
Tabia Za Kondoo.
1.
Wanamtegemea kabisa mchungaji wao. (Mwa.
4:2, 1Sam.17:20-28)
a.
Wanahitaji
i.
Kupelekwa malishoni
ii.
Kupumzishwa wachokapo
iii.
Kuponywa majeraha pindi wapatapo majeraha.
2.
Wanautambuzi hafifu sana kuhusu mwelekeo.
(Zab.119:176, Isa.53:6, Yer. 50:6, Eze. 34:12)
a.
Wakiachwa pekee,
hutangatanga na kupotea njia.
b.
Hawawezi hata kurudi
nyumbani peke yao.
3. Wanao
uwezo mdogo sana wa kujilinda wenyewe. (Mt.10:16,
Hes.32:24)
a.
Hawana hata kucha kali au
meno
b.
Hawawezi kukimbia haraka
sana
c.
Wakiachwa pekee ni rahisi
kuvamiwa na wanyama wa mwituni. Math10:16
4. Wanao
uwezo wa kumsikia na kumfuata mchungaji wao – Kondoo husikia sauti Ya mchungaji – Yoh 10:3 – 10
5.
Wanatoa - maziwa, sufu, na nyama.
Maana Ya Mchungaji
Poimen =
aangaliaye, atunzaye, aongozaye, na alilishaye kundi.
Poimaino = kuangalia, kutunza, kuongoza, na kulilisha kundi.
Uchungaji.
1. Uongozi.
a.
Kujiangalia Wenyewe - kuwa na uweozo wa kujilisha kupitia Roho Mtakatifu
b.
Kuliangalia Kundi
c.
Kufanywa Na Roho Mtakatifu
d. Kuangalia
e. Kuliona
Kanisa Ni Mali Ya Mungu
2. Huduma Ya Mchungaji
a.
Kulitunza kundi, kulilisha, kulinywesha, kulilinda kundi la kondoo
b.
Kujitoa mwenyewe kwa huduma ya unyenyekevu, kwa ajili ya hali njema ya kundi –
kuwa tayari hata kufa! “ Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili
ya kondoo” (Yoh. 10:11-15, 21:15
– 17, Ufu. 7:17)
c.
Mchungaji aongozwaye na Roho Mtakatifu ni kiongozi – mtumishi
d. Huduma
ya mchungaji ni kusaidia kuwaongoza watu kwenye uhusiano wa kiundani na BWANA/
MUNGU; wala sio:-
i.
Kuwatawala
ii.
Kuchukua nafasi ya uhusiano wa mwamini na Mungu; Ndio maana ya kupasuka kwa
pazia la hekalu (Mt.27:51) Hakuhitajiki
watu wa Mungu kuwakilishwa na ukuhani wa kibinadamu, Waamini wote waweza
kumwendea Mungu moja kwa moja.
3. Kristo Yesu – Kielelezo Cha Mchungaji.
a. Kanisa
ni watu wanaotawaliwa na Mungu – wana uongozi wa Kimungu (theocracy)
b. Mungu
ni Mchungaji (Mwa.49:24, Eze 32:12-14)
kwa Israeli.
i.
Huwaongoza (Zab.23:3)
ii.
Huwalisha (Yer.50:19)
iii.
Huwaongoza na kuwanywesha (Zab.23:2,
Isa.40:11)
iv. Huwalinda
(Zab.23:2, Isa. 40:11)
v.
Huwaita na kuwakusanya (Isa. 56:8, Zek.
10:8)
vi.
Huwabeba wanakondoo kifuani mwake (Isa.
40:11)
Vii.Huwaongoza
kwa upole wale wenye watoto (Isa.40:11)
c. Yesu
Kristo aliivaa sura ya Mungu. Ni Mchungaji Mkuu (1Petr.5:4)
i. Mfano
wa moyo wa kichungaji.
ii.
Wachungaji watendaji chini ya Mchungaji Mkuu, Yesu, wajifunze kwa uangalifu
moyo na msukumo wake, ili wafanane naye.
iii. Kila
mchungaji awe na moyo wa kichungaji wa Yesu Kristo. Aliwapenda na kuwahurumia
watu wa Mungu. (Mk.6:34) Alimthamini
sana kila kondoo. (Luk. 15:4). Alikuwa
tayari kuutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo (Yoh.10:11,15)
4. Sifa za huduma ya Kichungaji.
a. Aweze
kuongoza kondoo (Yoh.10:4)
i. Awe na
uhusiano na kutembea na Mungu binafsi kabla ya kuwaongoza wengine katika njia
za Mungu.
ii.
Akitaka watu wawe waombaji, watoaji, wasomaji wa neno, na watembeleaji watu,
lazima awe mfano.
iii.
Aishi maisha ambayo kondoo watayafuata. (1Kor.11:1,
Ebr. 13:7, 1Petr.5:23)
b. Aweze
kulilisha kundi. (Yer.3:15,23:4,
Eze.34:1-3, Mdo. 20:28, 1Petr.5:2-3)
i. Awe kwanza ndani ya neno na neno ndani yake.
ii. Inahitaji maombi, kusoma, kufikiri, na kuwa mtendaji wa
neno. (Yer. 10: 2, Mdo. 6:4)
c. Aweze
Kuhubiri na kufundisha katika urahisi na uwazi ili kila mtu aelewe.
Kualika wahubiri, semina, mikutano ya injili, …
d. Awe tayari kuutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. (Yoh.10:15, 3:16, Ufu. 12:11)
i. Kujitoa kwa ajili ya watu wa Mungu, kwa: Kuumimina uhai wake
na nguvu (kufunga na kuomba)
ii. Kuwatunza kondoo nyakati za uhitaji. (Eze. 34:4, Yoh. 10:13).
iii. Kukaa na kondoo nyakati za taabu. (Yoh. 10:12) Kutembelea nyumba za kondoo. (Zek.10:2,3)
iv. Kukesha
kwa ajili ya usalama wa kondoo (Ebr.13:7)
5. Huduma Ya Mchungaji/ Kazi Za Mchungaji
1.
Kuwatafuta Kondoo waliopotea. (Luk.15:4)
2.
Kukesha kwa ajili ya mambo yatakayolidhuru kundi;-
a. Mbwa mwitu wakali
b. Waalimu wa uongo.
3. Kuwajali
wahitaji wa: - (Yoh. 10:11-13)
a. Kiroho
b. Kimwili
i. Kifamilia, shule, na maeneo mbalimbali ya maisha.
ii. Faraja na ushauri kwa wagonjwa, wafao, viwete, masikini,
wajane, yatima, na wenye kuumia.
4. Kuwarekebisha waliokosea (Zab. 23:4)
a. Fimbo ya mchungaji hutumika kuwafikia na kuwaokoa kondoo waliopotea.
b. Gongo hutumika kuwalinda wakiwa hatarini na pia kuwarekebisha wapoteao na
waasi wasiosikia.
Maonyo Kwa Wachungaji
1. Asipuuzie au kutojali kukua kwake binafsi kiroho. (Yer.2:8, 1Tim. 4:15,16)
a. Kuutumia muda mwingi wa kuwa na mchungaji Mkuu.
b. Wanahitaji ulinzi kwani yeye ni lengo la kwanza la shetani. (Zek.13:7, Mat 26:31)
2. Asifanye kazi hii kwa faida yake binafsi. (1Tim.
3:3, 1Petr. 5:) sura yote, Yoh
10:1-13
i. Mwivi
ii. Mnyang’anyi
iii. Mtu wa mshahara.
3. Asitafute nguvu za kiulimwengu. (Eze. 34:4, Luk. 22:24-27, 1Pet.5:3)
i. Kama vile
1. Siasa 2. Uongozi /utawala wa duniani
4. Asiwaendeshe kondoo (Mwa.33:13). Awe mvumilivu kwa kondoo,
asije akawaacha wengine nyuma.
5. Adumishe familia ya kibiblia (Efe.5:25)
a. Mambo ambayo Mungu ameyaweka ili mtu ayape
kipaumbele.-ayajali, kwanza ni:-
i. Uhusiano wa mtu na Mungu. (Yoh.15:5)
ii. Wajibu wake katika familia ya:
1. Nyumbani. 2. Watu wa Mungu –Kanisani. Efe.5:25, 33; Tito 2:4; 1Tim 3:5; 5:8)
iii. Kwa wengine.
Hukumu Kwa Wachungaji
Wasio Waaminifu.
1.
Kunyang’anywa kondoo na
kupewa wachungaji wale walio waaminifu. Waamini kuhama makanisani (Yer.10:21; 23:1-4)
2. Kuwa chini ya mkono wa Mungu wa hukumu nzito (Yer.10:10 13;22:22,23:1-5; 25:34-38; 50:6-7; Zek. 10:3;11:17;
Mdo.20:28-38)
5.
Karama Ya Huduma Ya Mwalimu (Mt. 28:19 – 20)
Ni muhimu katika
uanzishwaji wa kanisa.
Maana ya Mwalimu ;-
Didasko = kufundisha au
kuelekeza, Ni njia ya kuelezea kitu.
Mwanzo Wa Walimu Katika
Biblia;
1. Wazazi
2. Musa
3. Waandishi.
Kristo Yesu – Kielelezo Cha Mwalimu (Yoh. 3:2, 13:13)
Alifundisha kwa nguvu na mamlaka na upako wa Roho Mtakatifu. (Mt.7:28 29) Maneno yake yalihusu sana
Baba yake na kazi za Roho Mtakatifu. Hii ilikuwa ni ufunguo wa huduma yake, pia
kwa yeyote leo mwenye huduma ya Ualimu, atakaye kufanikiwa katika kazi ya
ualimu wa neno la Mungu.
Viwango Vya Walimu
1. Kila Mwamini anatakiwa kuwafundisha wengine kuhusu maisha ya
kikristo. (Mt.28:20, Kol. 3:16), hii
haina maana kwamba kila mwamini ni mwalimu katika kanisa bali wapo waliopewa
huduma hii kwa Neema.
2. Kila Mzazi Na Kila Mzee anatakiwa aweze kuwaelekeza wengine
katika njia ya Mungu. (1Tim 3:2)
Karama Ya Huduma Ya
Ualimu Katika Kanisa.
a. Ni mojawapo ya karama
za huduma tano; itendayo kazi katika kanisa (Efe.4:11, 1Kor. 12:28-29)
b. Paulo inaonekana alikuwa Mwalimu kabla ya kuwa Mtume. (Mdo 11:26; 2Tim1:11).
Wakati ambao
hakuwa katika Huduma ya Kitume, alirudi na kuwa tena Mwalimu kanisani. (Mdo.15:35)
c. Kulikuwepo na walimu wengine Antiokia. (Mdo13:1)
d. Waliiona kuwa ni huduma muhimu na waliijali sana katika kanisa
(Yak.3:1)
Viwango Au Aina Za Ufundishaji
(Kuhubiri Au Kusema Neno La Mungu) (1kor.14:6).
Kufundisha Kwa
a. Mafunuo (Revelations)
b. Ujuzi / maarifa (Knowledge)
c. Kifuniko cha Roho / cha Unabii
d. Mafundisho (Doctrine)
Maelezo Maalumu Kuhusu Karama Ya Huduma Ya Mwalimu.
1. Upo uhusiano wa karibu sana kati ya huduma ya mwalimu na
huduma ya mchungaji.
2. Huingiliana, japo kuwa si huduma moja.
3. Huduma ya mwalimu na ya mchungaji zinategemeana.
4. Mwalimu ashirikiane na mchungaji au Wazee wa kanisa katika
kazi ya kuwaadibisha waamini.
5. Mchungaji awatie moyo wale wenye huduma ya Ualimu.
6. Kama nabii, Mwalimu naye anahitaji upako wa Roho Mtakatifu,
lakini nabii huendeshwa na Roho Mtakatifu katika uvuvio zaidi au hali ya
kutojiandaa (papo kwa papo).
7. Mwalimu mwenye upako hutenda kazi katika njia ya kipimo zaidi
kwa udhahiri katika kuangazia kweli za neno la Mungu kwa namna nyepesi ya maelekezo
na Ufahamu.
Mambo muhimu katika
Huduma Ya Mwalimu.
Maeneo muhimu kuhusu huduma ya kufundisha.
Mwalimu anatakiwa awe na yafuatayo:-
1. Asiache kujifunza na kujiandaa. Yapo mengi ya kujifunza
katika shule ya Roho Mtakatifu. (1Kor.2:13)
2. Alifahamu Neno la Mugu. (Mk.12:24).
Hawezi kufundisha asicho kifahamu au asichowahi kukitumia katika maisha yake.
a. Aweze kuitumia kweli ya biblia katika hali za kimaisha. (Mk.9:14-29)
b. Aweze kuweka msingi imara wa waamini wapya. (Ebr.5:12)
3. Aweze kufundisha kwa mifano (Yoh.13:13-14)
a. Kwa kuishi maisha sawa na yale ayafundishayo, vinginevyo
itakuwa ni unafiki. (Mt.23:1-3; Mdo1:1)
b. Ujumbe mkuu wa mwalimu ni jinsi alivyo yeye mwenyewe wala si
asemavyo!
4. Afundishe kwa usahihi na kwa kueleweka. (2Tim.2:15)
a. Anabeba wajibu wa kufundisha kwa usahihi.
5. Atafute kuwaleta wengine katika kiwango cha ufahamu alionao
yeye. Mt.10:24-25; Mdo.20:20, 27)
6. Thawabu kubwa ya mwalimu ni kuona kuwa maisha ya wale awafundishao
yanabadilishwa kwa neno la Mungu na kwa nguvu za Roho Mtakatifu. (Kumb.4:5, 14; 31:12-13)
a. Neno la Mungu hutenda miujiza ya nguvu sana pale
linapofundishwa, linapopokelewa, na kulitii.
7. Asaidiwe na wale anowahudumia:
a. Ili aifanye huduma kwa wakati wote.
b. Inahitaji maombi, kusoma, kujiandaa, na kufundisha Neno.
c. Ni kazi iliyo ngumu, si kirahisi rahisi tu!
Maonyo Kuhusu Waalimu Wa Uongo.
Walimu
hugusa mioyo na akili za watu. Hapandikiza tu kweli na habari, bali mwelekeo na
tabia. Mwalimu anao uwezo wa kutengeneza umbile na kuutawala mwelekeo wa
wanafunzi kwa mema sana au mabaya sana. Kwa ajili hiyo, Mungu anawaonya watu
wake wajiepushe na waalimu wa uongo.
Aina Za Walimu Wa Uongo Ni kama ifuatavyo:-
1.
Wafundishao yaipotoshayo kweli (ya uongo)- Yasiyopatana na mashauri mazima ya
Mungu. (2Tim.4:3-4; 2Petr.2:1)
a. Yaipingayo / yaliyo kinyume na Kweli. (2Pet. 2:1; Isa.8:20)
b. Yaiongezeayo kweli / Yazidiyo kweli. (Ufu. 22:18, Mt. 5:37; 2Kor.1:17; Yak. 5:12)
c. Kuipunguza kweli (Ufu.22:19)
Sababu ya ubinafsi na tamaa za nafsi zao katika mioyo yao.
2.
Wafundishao Mapokeo ya wanadamu kama neno la Mungu. (Mk.7:7)
a. Mawazo
na matendo yao.
b. Mila
na desturi.
Usipokee
tu kila unachofundishwa na kukiamini bila kukipima kwa neno la Mungu kama ni
kweli! (Mdo. 17:11) na neno la Mungu
linasema tuzijaribu kila roho yaani tuzipime katika neno la Mungu ili tujue
kuwa ni za kweli.
2.
Wafundishao kwa nia mbaya
(1Kor.4:15) - Faida, Nguvu, cheo, (Tito 1:10-11; 2Pet.2:3).
Faida za Karama za Huduma Tano Na uhusiano na Wazee Wa Kanisa.
1. Mtume
–Huhitajika ili Kuongoza.
2. Nabii
– Huhitajika ili Kuonyesha mwelekeo
3.
Mwinjilisti - Huhitajika ili Kukusanya au kuvuna.
4.
Mchungaji – Huhitajika ili Kulinda au Kutunza.
5.
Mwalimu – Huhitajika ili Kujenga msingi / kufundisha.
Mtume na
Mwinjilisti – huhudumu pia mbali na kanisa la nyumbani - Huduma za kimisheni.
Nabii na mwalimu – huweza pia kusafiri, lakini wanayo kazi maalumu sana
nyumbani.
Mchungaji - huhudumu kanisani, lakini aweza kwenda katika huduma za kimisheni.
Mamlaka Ya Wazee Wa Kanisa
Mandiko
hayaonyeshi uhusiano wa moja kwa moja kati ya Huduma tano na wazee wa kanisa.
Zipo
kweli kadhaa zinazo onyesha uhusiano wake.
1. Agano
Jipya halitaji kamwe neno huduma tano. (Ila Efe.4:11; 1Kor. 1Kor.12 :)
a. Ni
karama za huduma sio ofisi (ofisi ina maana watu huhusika katika kupiga kura au
kuchagua na kisha kuwasimika viongozi au mawakili katika huduma fulani)
b. Ni karama
za maongozi / maangalizi.
2. Zipo
osisi za aina mbili tu katika Agano Jipya (Fil.1:1)
a. Wazee
wa Kanisa
b.
Mashemasi. (1Tim.3:1-15)
3.
Maandiko Hutaja tu wazee “Kusimikwa” kwa maombi kufunga na kuwekewa mikono.
4. Wazee
hushika nafasi ya wajibu na mamlaka katika kanisa. (1Tim. 5:17, Mdo. 20:17; 21:18-19; 11:30)
5. Baadhi
ya Waliopo katika huduma tano huweza kusimikwa kuwa wazee wa kanisa.
a.
Mchungaji ndiye Mkuu wa wazee wa kanisa- “Mzee kiongozi”.
b. Baraza
la wazee wa kanisa latakiwa liwe na Mchungaji, Nabii, na Mwalimu- ili liwe na
utendaji mzuri.
i.
Mchungaji anatakiwa awe na;-
1. Moyo
wa kichungaji
2. Maono
ya kiunabii
3. Hekima
ya mwalimu
c. Hata
Mtume, Mwinjilisti, Nabii au Mwalimu lazima awe na kanisa la Nyumbani atokako!
TABIA ZA MASHEMASI – [1Timotheo 3:8-13.]
1) Ujazo
wa Roho Mtakatifu
2) Mwenye
upendo kwa kanisa
3) Kuwa
na msimamo – mwenye kauri moja na ile ya Neno la Mungu, mchungaji pamoja na
wazee wa kanisa.
4) Mwenye
uamuzi mzuri, bila ya kigeugeu.
5) Wasio
na tamaa wala choyo (kuhusu pesa na mali)
6) Wenye
imani na uwezo wa kuitetea imani.
7) Wenye
dhamiri safi
8) Wasiio
na hatia – wenye maisha safi.
9) Wenye
ndoa takatifu (mme na mke mmoja).
10)
Wawezao kufundisha na kuelekeza wengine.
11)
Kukubalika / kutokulaumika
12) Wenye
kiasi (kujitawala) na busara
13) Wenye
kufuata utaratibu (mpangilio/ratiba na kanuni)
14)
Ukarimu (ukaribishaji)
15) Wenye
kujua kufundisha (mwalimu)
16) Si
mtu wa kujadiliana (Mbishi)
17)
Mwenye kuisimamia nyumba yake vizuri – mwenye sifa nzuri nyumbani.
18) Asiwe
mchanga kiroho.
19)
Mwenye ushuhuda mzuri kwa wasioamini pia.
20)
Mwenye kupenda kutumikia na si kutumikiwa.
KAZI ZA MASHEMASI
1)
Kusimamia taratibu zote za kikanisa, kama vile
a) Usafi na upambaji wa kanisa
b) Kupanga ukaaji wa watu kanisani
c) Ulinzi wa kanisani wakati wa ibada
d) Kusimamia upishi na uugawaji wa vyakula
e) Kuwakarimu wageni - kuwapokea, kuwakaribisha, kupata taarifa
zao na kuwapa maelekezo.
f) Kuwahudumia wagonjwa na wasiojiweza
g) Kuwasaidia wanaodondoka na wenye mapepo wakati wa maombezi
h) Kusimamia ratiba za kikanisa.
2) Kusimamia
waamini wa mtaani kwako
a) Kusimamia ibada za nyumba kwa nyumba
b) Kuwahudumia washirika walio wajane, yatima, wagonjwa na
wasiojiweza.
c) Kusaidia mawasiliano ya kikanisa wakati wa ibada na hata
wakati mwingine.
d) Kufuatilia taarifa za washirika.
3)
Kufundisha, kuonya, na kuelekeza na kuwatia moyo washirika.
4)
Kushirikiana na kufanya kazi kwa upendo pamoja na mchungaji na wazee wa kanisa;-
a) Kusaidiana pamoja na wazee wa kanisa katika kusimamia kazi za
kanisa.
b) Kutunza pesa na mali za kanisa pamoja na kumbukumbu za
kanisa.
c) Kusimamia na kuhimiza utekelezaji wa maagizo ya kanisa la
mahali;
d) Kusimamia na kuhimiza utekelezaji wa maagizo toka ngazi za
juu.
e) Kujitoa kwa hali na mali, ili kuifanya kazi ya Mungu.
5) Kuwa
mshauri wa mchungaji na wazee wa kanisa.
6)
Kuliombea kanisa.
7)
Kuiombea, kuihudumia, na kuitunza nyumba na familia ya mchungaji.
WAZEE WA KANISA. TABIA ZA
WAZEE WA KANISA. [1Tim. 5:17, Mdo. 20:17; 21:18-19; 11:30; 1Timotheo 3:1-7]
1) Ujazo
wa Roho Mtakatifu
2) Mwenye
upendo kwa kanisa.
3) Kuwa
na msimamo – mwenye kauri moja na ile ya Neno la Mungu, pamoja na
Mchungaji
4) Mwenye
uamuzi mzuri, bila ya kigeugeu.
5) Wasio
na tamaa (ya pesa)
6) Wenye
imani na uwezo wa kuitetea imani.
7) Wenye
dhamiri safi
8) Wasiio
na hatia – wenye maisha safi.
9) Wenye
ndoa takatifu (mme na mke mmoja).
10)
Wawezao kufundisha na kuelekeza wengine.
11)
Kukubalika / kutokulaumika
12) Wenye
kiasi (kujitawala) na busara
13) Wenye
kufuata utaratibu (mpangilio/ratiba na kanuni)
14)
Ukarimu (ukaribishaji)
15) Wenye
kujua kufundisha (mwalimu)
16) Si
mtu wa kujadiliana (Mbishi)
17)
Mwenye kuisimamia nyumba yake vizuri – mwenye sifa nzuri nyumbani.
18) Asiwe
mchanga kiroho.
19)
Mwenye ushuhuda mzuri kwa wasioamini pia.
20)
Mwenye kupenda kutumikia na si kutumikiwa.
KAZI ZA WAZEE WA KANISA
Ni
watendaji wakuu wa shughuli zote za kikanisa
a)
Kuliombia kanisa
b)
Maangalizi ya kanisa
i) Kusimamia taratibu zote za kikanisa, kama vile;-
(1) Usafi na upambaji wa kanisa
(2) Kupanga ukaaji wa watu kanisani
(3) Ulinzi wa kanisani wakati wa ibada
(4) Kusimamia upishi na uugawaji wa vyakula
(5) Kuwakarimu wageni - kuwapokea, kuwakaribisha, kupata taarifa
zao na kuwapa maelekezo.
(6) Kuwahudumia wagonjwa na wasiojiweza
(7) Kuwasaidia wanaodondoka na wenye mapepo wakati wa
Maombezi
(8) Kusimamia ratiba za kikanisa.
ii) Kusimamia waamini wa mtaani kwako
(1) Kusimamia ibada za nyumba kwa nyumba
(2) Kuwahudumiawashirika walio wajane, yatima,
wagonjwa na wasiojiweza.
(3) Kusaidia mawasiliano ya kikanisa wakati wa ibada na
hata wakati mwingine.
(4) Kufuatilia taarifa za washirika.
(5) Kufundisha, kuonya, na kuelekeza na kuwatia moyo
washirika.
iii) Kushirikiana na kufanya kazi kwa upendo pamoja na mchungaji ambaye ndiye
kiongozi katika Wazee
(1) Kuwa washauri wa mchungaji
(2) Kufundisha na kuhubiri Neno la Mungu.
(3) Kuongoza- kuelekeza kinachotakiwa kufanyika na kuweka utaratibu wa kazi
(4) Kuwatunza washirika wasipotee
(5) Kupima na kutathimini matokeo na kiwango cha utekelezaji
(6) Kusimamia mipango ya kanisa ili matokeo yake yawe mazuri
(7) Kuviangalia na kuvitunza vitu vyote vya kanisa
(8) Kuwa mbunifu na karibu sana na mchungaji katika kupanga mipango
mbalimbali na kuangalia matokeo yake,
(9) Kusaidiana pamoja na mchungaji katika kusimamia kazi za kanisa.
(10) Kusimamia na kuhimiza utekelezaji wa maagizo ya kanisa la
mahali;
(11) Kusimamia na kuhimiza utekelezaji wa maagizo toka ngazi za
juu.
(12) Kujitoa kwa hali na mali, ili kuifanya kazi ya Mungu.
(13) Kuwaadibisha washirika weye mwenendo usio sahihi.
(14) Kuongoza ibada ya mazishi (kwa kibali cha mchungaji kama
ikibidi)
iv) Kutunza pesa na mali za kanisa pamoja na kumbukumbu za
kanisa.
2)
Kuiombea, kuihudumia, na kuitunza nyumba na familia ya mchungaji.
a) Kuwa msemaji wa mahitaji, utunzaji na kuitegemeza nyumba na
familia ya mchungaji - kwa kanisa.
HITIMISHO
Ni muhimu
sana kwa kila mwamini aliyeokoka kutambua huduma yake aliyopea na Mungu na
kuifanyia kazi kwa moyo mkuu bila ulegevu, kwani kwa kufanya hivyo tutaujenga
mwili wa Kristo ambalo ndilo kanisa alilolinunua kwa damu yake ya thamini na
kulitolea uhai wake. Kwani biblia inaweka wazi kuwa “amelaniwa mtu Yule aifanyaye kazi
ya Bwana kwa ulegevu. Kila mmoja wetu baada ya kukoka Mungu ameweka
huduma fulani ndani yake ili kusudi alitumikie kusudi la Mungu katika Kanisa.
Mungu awabariki kwa viwango vya juu.
Mwl. Musa Festo
Contacts: mussafesto@gmail.com
+255675415262
Comments
Post a Comment