HISTORIA YA MAISHA YA MITUME 12 WA YESU
Maisha ya Mitume/ wanafunzi wa kristo na wajibu waliopewa na Yesu kristo baada ya kristo kuondoka. Lengo hasa ni kutuwezesha kujua namna ambavyo waliotutangulia katika wokovu walivyokutana na changamoto ili na sisi tupige mbio zaidi katika kuutangaza ufalme wa Mungu.
Hii ni kwa kuwa tumepokea hiki kijiti toka kwao hivyo na sisi tunayo safari yetu katika kristo YESU.
Habari kuhusu Maisha ya Mitume hao na namna walivyosambaa duniani kote mpaka vifo vyao zinapatikana katika vitabu vilivyoandikwa katika kanisa la Kwanza. Schumacher ni Mwanahistoria wa kanisa aliyefanya utafiti kuhusu maisha ya mitume (wanafunzi wa kristo) na hivi ni namna ambavyo mitume hao walivyokumbana na misukosuko katika kumtangaza Kristo Yesu.
1. MATHAYO
Huyu alikuwa mkusanya kodi (mtoza ushuru) kabla ya kumfuata Yesu. Mathayo ndiye alieandika kitabu cha Mathayo Mtakatifu. Alihubiri na kusambaza neno la Mungu huko Persia na Ethiopia ya sasa. Aliuawa kwa upanga baada ya kugoma kuacha kuhubiri neno la Mungu huko Ethiopia.
2. MARKO
Marko yeye alifia katika mji wa Alexandria kwa sasa ni Misri. baada ya kuburutwa na Farasi katika mitaa ya mji huo mpaka mauti ilipomfika kwa sababu hakupata msaada
3. LUKA
Huyu ndiye alieandika Injili ya Luka Mtakatifu, na pia mwandishi wa kitabu cha Matendo ya mitume mbali na kuhubiri Neno la Mungu alikuwa ni Tabibu . Aliuwawa kwa kunyongwa mwaka 84 baada ya Kristo (AD) huko Ugiriki, hii ni kutokana nĂ msimamo wake mkali aliouonesha juu ya ukristo
4. YOHANA
Huyu alitumbukizwa katika pipa[kikaango/sinia] lenye mafuta yanayochemka huko Roma, Italia ya sasa. Hata hivyo kwa miujiza hakuungua na alitolewa akiwa mzima kabisa. Alipelekwa katika gereza lililokuwa katika migodi huko kisiwa cha Patmos. Na huko ndiko alipofunuliwa na mwenyezi Mungu na kuandika kitabu cha "Ufunuo wa Yohana". Baadae aliachiwa huru na kwenda kutumika kama askofu huko Edessa, Uturuki ya sasa. Alifariki akiwa mzee sana. Yohana alifariki akiwa mzee sana na ni mwanafunzi wa kristo pekee aliyekufa pasipo mateso.
5. PETRO
Yeye baada ya kukamatwa akieneza Injili ya Kristo, aliamriwa asulubiwe juu kama Kristo Yesu, Lakini petro aliwaomba watu hao wamsimsulubishe kama ambavyo kristo alifanyiwa kwa kua Petro alisema yeye hana hadhi ya kusulubishwa kama Bwana wake. Ndipo walipoamua kumsulubisha kinyume na Kristo, hivyo Petro akasulubiwa kichwa chini miguu juu mpaka mauti ilipomfika kwenye msalaba.
6. YAKOBO [JAMES]
Alikuwa Kiongozi wa kanisa huko Jerusalemu, Israel ya sasa. Yeye alitupwa kutoka juu kabisa ya mnara wa hekalu wenye urefu wa meta 100 baada ya kutataa kuikana imani ya kristo yesu (mnara huo ndio ule ule ambao shetani alimjaribu Yesu kwa kumwambia kama yeye ni mwana wa Mungu ajirushe). Walipogundua kuwa hajafa baada ya kumdondosha toka juu ya kinara hucho , maadui walimpiga na mawe [nondo/rungu] mpaka akafa.
7. YAKOBO MWANA WA ZEBEDAYO [JAMES]
Akiwa kiongozi mkubwa wa kanisa huko jerusalemu pia , Alikuwa ni mvuvi kabla Yesu hajamteua kuwa mwanafunzi/mtume wake. Yakobo aliwekwa gerezani kwa sababu ya msimamo wake wa Imani juu ya kristo. Maajabu ni kwamba askari aliyekuwa akimlinda huko gerezani alishikwa na mshangao mkuu, jinsi yakobo alivyoshikiria msimamo wake wa kuhubiri Neno la Mungu wakati wa hukumu. Baadae yule askari alienda akapiga magoti mbele ya Yakobo na kiikiri Imani yake mpya juu ya kristo. Na ndipo wote walichinjwa mbele ya kadamnasi ya watu, hivyo Yakobo mwana wa zebedayo aliuwawa kwa kuchinjwa
8. BATHOLOMAYO
Alijulikana kama Nathanieli. Alikuwa ni mmisionari katika bara la Asia. Alimshuhudia Yesu kristo huko Uturuki. Yeye aliuawa kwa kukaangwa baada ya kugoma kuacha mafundisho yake ya Neno la Mungu.
9. ANDREA
Yeye alitundikwa msalabani kwa mfumo wa X katika mji wa Patras nchini ugiriki baada ya kuteswa ipasavyo na askari wapatao saba, kasha wakamfunga msalabani with cords to plorong his agony. Wafuasi wake walisema wakati wanampeleka msalabani, Andrea alisema “Nina uamuzi udumuo na niliutegemea muda huu wa furaha”. Aliendelea kuhubiri akiwa hapo msalabani kwa siku mbili mpaka pumzi yake ya mwisho ilipokoma, kwa hiyo Aliuawa kama Petro.
10. THOMASO
Huyu alihubiri Neno la Mungu huko Syria, China na baadae India. Huko India alianzisha kanisa liitwalo Mar Thoma. Kanisa hili lipo mpaka leo huko India. Yeye aliuawa kwa kuchomwa na mkuki [mshale] na maasikari wanne huko India alipokua katika moja ya safari zake za kiumishieni kwa ajili ya kufungua kanisa.
11. YUDA (sio eskariote)
Nae pia alipigwa na mshale.
12. MATHIAS
Mwanafunzi aliyepigiwa kura na wanafunzi wa Yesu kuziba nafasi ya Yuda eskariote msaliti. Huyu alipigwa na mawe hadi kufa na baada ya hapo walimkata kichwa.
13. PAULO
Aliteswa na baadae akachinjwa na mfalme Nero huko Roma tarehe 9 mwezi june mwaka 68 Ano Domino (A.D). Ila mfalme Nero nae alijiua mwaka huo huo. Paulo aliishi muda mrefu sana gerezani ambapo akiwa huko aliandika barua(waraka) nyingi kwa makanisa ya Roma. Ndio hizi ambazo zinafundisha misingi ya ukristo katika agano jipya, kama vile Waraka wa Paulo mtume kwa Warumi, Wakoritho, Waefeso, Wakolosai, Wathesalonike, Timotheo etc.
Inawezekana huu ni ukumbusho kwetu kwamba mateso tunayopitia ni madogo sana ukiringanisha na haya ambayo mitume waliyapitia. Yote ni kwa ajili ya kutetea kanisa la Mungu. Ajabu siku hizi watu wamegeuza dini ya kikristo kuwa sehemu ya upigaji wa hela kutoka kwa watu maskini na kujigeuza kiimani baada ya dhoruba ndogo tu ya kimaisha ikiwemo kukosa ndoa ya kikristo.
Angalizo;
"Naanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu, lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka." Mathayo Mtakatifu 10:22
•》IKUMBUKWE KUWA.
MARKO; LUKA na PAULO hawa siyo miongoni mwa MITUME 12 wa YESU KRISTO
Japo kuwa Historia yao Imeweka kwa faidaa yako msomaji.

Comments
Post a Comment