SIRI YA UPONYAJI

SOMO: SIRI YA KUPONYWA


UTANGULIZI

Tunaposema juu ya uponyaji na kufanikiwa haina maana juu ya uponyaji wa aina moja tu, yaani uponyaji wa mwili tu.
Biblia inaposema uponyaji ina maana katika maeneo matatu yaani;
1. Uponyaji wa Rohoni
2. Uponyaji wa Nafsi
3. Uponyaji wa Mwili
3 Yohana 1:1 – 2 “Mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli. Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo”
Efeso 1:3 “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa Baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo”.
Zaburi 103:3 – 5 “Akusamehe maovu yako yote, akuponya magonjwa yako yote, aukomboa uhai wako na kaburi, akutia taji ya fadhili na rehema, aushibisha mema uzee wako, ujana wako ukarejezwa kama tai”
2 Petro 3:17 “Basi, wapenzi mkitangulia kujua hayo, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuucha uthabiti wenu”.
2
Katika maandiko hayo uaona kuna maeneo matatu yahusuyo uponyaji yaani Rohoni (chanzo cha mambo yote), nafsi na mwili.
Hapo maandiko yanaonyesha wazi juu ya Baraka ambazo Mungu ameahidi kwetu na jinsi Mungu alivyo na uhakika juu ya yale aliyotuahidi, hivyo kama hayatimii kwetu au hayajatimia basi kuna kizuizi kinachoyazuia yasitimie kwetu. Na hii ndiyo siri yenyewe!!
HEBU TUNGALIE SIRI HIYO
Siri hii iko katika maandiko Matakatifu,tizama hapa mwana wa Mungu
Yakobo 5:9, 16 “Ndugu, msinung’unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango. Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii”
Kolosai 3:8 – 14 “Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu….. Basi kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake,kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu”.
chanzo cha uponyaji ni kuungamiana dhambi zetu sisi kwa sisi, kuombeana sisi kwa sisi. Kuungamiana ni tendo la kumwambia mwenzako mwenzako kile ambacho umemfanyia kisicho sahihi na
3
kuomba msamaha au kumsamehe.na hii ndiyo siri kuu ya kufanikiwa kwa mambo yako yote, yaani KUSAMEHEANA SISI KWA SISI, kwani msamaha ni kwa ajili yetu sisi wanadamu kwa kuwa Mungu hahitaji kusamehewa wala kujisamehe kwani yeye hakosei wala hakosi hata kidogo.
Mara zote uponyaji lazima uanzie rohoni 3 Yohana 1:2 “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo”. Hivyo basi kama rohoni kuna matatizo basi mwili mzima una ugonjwa na utaathirika kwani mafanikio na uzima wa mwili hujengwa rohoni yaani rohoni ndiko kwenye chemchemi za uzima (Mith 4:23). Kwa kuwa uponyaji wa rohoni ndiyo matokeo ya nje yanayoonekana. Kwa nafsi (Moyo), Roho vinakuwa vimeponywa, hivyo mtu huyo anafanikiwa katika mambo yote. Mathayo 9:2, Mith 4:20 – 23, Mith11:17.
Moyo wenye uchungu na kinyongo humfanya mtu kuwa mgonjwa, hali yako ya rohoni itadhihirisha afya yako ya nje.
Waefeso 4:31 “uchungu wote na ghadhabu na hasira na kele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya”. Hapa Mungu anatuagiza kuondoa uchungu ili kukaribisha uponyaji katika Nafsi, Roho na mwili ili tupate kufanikiwa.
Mfano mzazi ama mtu huwezi kubeba mtoto kwenye mbeleko moja na hiyo hiyo mbeleko ukabeba mawe kwa wakati huo huo, lazima mtoto
4
ataumia na jambo hilo halitawezekana, kwani nasi wokovu tulionao ni kama mtoto unahitaji kulelewa na mahali pa kuulelea ni rohoni kwani tunafanyika upya kwa jinsi ya rohoni, hivyo basi kuweka uchungu na ghadhabu, matukano na kelele ni kuumiza utu wetu wa ndani. Ndiyo maana andiko linasema uchungu na mambo yote yaliyoandikwa hapo juu tuyaondoe katika Nafsi, Roho na mwili ili Roho wa Mungu aingie tupate uponyaji na kufanikiwa.
HASIRA NA CHUKI.
Hasira husababisha chuki/kuchukia na hali hii ikiendelea huleta kelele na matukano ambayo husababisha fundo lenye kinyongo ndani, kwani Biblia inasema katika Efeso 4:26 “Mwe na hasira, ila msitende dhambi, jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka
Napenda mstari wa 27 anasema wala msimpe Ibilisi nafasi. Kumbe kuwa na hali ya kuhifadhi kinyongo ni kumpa ibilisi na majeshi yake yaani mapepo nafasi ndani yako. Hii inaonyesha wazi kuwa unapokwazwa lazima uwe na kiwango cha kutofikia kutenda dhambi yaani kujizuia na kuachilia.
Mfano unaweza kumchukia ndugu/rafiki yako na kusema wa kazi gani huku ukiona hakuna lolote analoweza kukusaidia kumbe unajikomesha mwenyewe maana itakuletea maumivu moyoni. 1Yohana 3:15 “Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji, nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji
5
hana uzima wa milele ukikaa ndani yake”. Napenda pale juu mstari wa 14 unaposema Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. Yeye asiyependa, akaa katika mauti.
NAMNA YA KUFANYA
1. Ukiona umekwazwa usitafute mtu wa kumshirikisha makwazo yako, bali nenda moja kwa moja kwa aliyekukwaza na ukaongee naye vizuri kama ndugu ili kutafuta suluhu na aliyekukwaza maana mambo ya kukwaza hayana budu kuwapo, lakini Bwana YESU alisema ole kwa mkwazaji na mkwazwaji. Luka 17:1 – 4.
2. Tunapaswa kuwa na kiasi katika mambo yote hasa tunapoona kile kinachokuwa kinamkwaza ndugu yako, kiache (kata mkono) maana ni heri kuingia katika uzima wa milele ukiwa na mkono mmoja kuliko jehanam ya milele ukiwa na mikono miwili. Kubali kupata hasara kwa ajili ya mwenzako, yaani kuumia kwa nduguyo mumeo, mkeo, mtoto wako n.k ili mradi ni mwanafunzi wa Bwana YESU, anaumia YESU hivyo utakuwa umefungiwa jiwe shingoni. Kuna watu wamefungiwa mawe shingoni ila bado kutupwa baharini, lakini hawajijui kama wamefungiwa mawe shingoni kwa ajili ya mambo ya kukwaza.
6
3. Kujinyenyekeza
Math 18:4 – 5
Hali hii hutokana na mtu kutotaka kujinyenyekeza chini ya mkono wa Mungu na kuwa kama mtoto mdogo, mtoto anatabia ya kukosewa na muda huo huo husahau, na kuanza kucheza na mwenzie aliyemkosea au kuadhibiwa na mzazi wake, haweki adhabu hiyo moyoni bali huona kama sehemu ya maonyo juu ya makuzi yake. Katika andiko la 1Petro 5:6 Mungu anatuagiza tujinyenyekeze chini ya mkono wake na kumkabidhi mambo kwa namna Fulani ni matatizo yanayotusumbua yatokanayo na kuumizwa na watu ili yeye ayashughulikie na kutuponya roho, nafsi na mwili ili tupate kufanikiwa. Kwa kuwa watu wengi leo wanajikuta wakiugua magonjwa ya vidonda vya tumbo, presha, moyo kwa sababu ya kutotaka kuachilia, ikiwa chanzo ni kuumizwa kwa mabaya waliyofanyiwa baada ya kuyaweka sana moyoni na kufanya uchungu wa muda mrefu.
BAADHI YA DALILI ZA KUFUNGIWA JIWE SHINGONI
i. Mambo yako yanakuwa hayaendi kama unavyotaka kila jambo linakuwa zito na yanaharibika bila kutegemea.
ii. Mara nyingi mambo yanapokwenda kinyume na matarajio yako unaponung’unika, tu tayari unafungiwa jiwe shingoni.
7
Yakobo 5:9 “Ndugu, msinung’unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni mwamuzi amesimama mbele ya milango”. Mhubiri 5:6 “Usikiache kinywa chako kuukosesha mwili wako”.
iii. Kuwa na hali ya kutotaka suluhu yoyote kwa mtu yoyote.
KANUNI ZA MSAMAHA
i. Msamaha siyo tendo la kuhisi ila ni la kudhamiria toka ndani au kwene kilindi cha moyo wako wote. Hebu angalia na kujifunza kwa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni mkombozi na mwanzilishi wa Imani yetu Luka 23:34 “Yesu akasema Baba uwasemehe kwa kuwa hawajui watendalo”. Pia tunasoma na kujifunza habari za Stephano alivyotoa msamaha toka ndani, japo alikuwa akishambuliwa kwa mawe Matendo 7:59 – 60 tunapaswa pia kujifunza kwa Yusufu Mwanzo 45:3 – 5.
Watu wengi husema nimekusamehe lakini ndani wanasema sintosahau hali hii ni hisia tu (emotion) na siyo msamaha wa dhati ya moyo, ndiyo maana akikosewa mtu wa namna hii hukumbuka nay a nyuma na kuanza kuyafanyia kazi wakati huo. Jifunze pia hapa kwa Elisha 2Wafalme 6:16 – 23
ii. Msamaha wa kweli na wa Kimungu ni ule utakaozungumza ukweli na ndugu ambaye mmekoseana naye siyo kusema
8
kimoyomoyo ndiyo maana ukisamehe kimoyomoyo bila kuzungumza naye, fundo la uchungu hubaki moyoni, kwa kuwa ukitamka (kuzungumza) ni kukiri na unaondoa sumu ya uchungu moyoni na kuachilia. Math 18:15 – 16, 1Samweli 24:1 – 15
iii. Mwombee rehema ili abadilike na apate kufanikiwa. Math 5:44 – 45.
MADHARA YA KUTOSAMEHE AU KUJISAMEHE
i. Ni kuwa na kinyongo, wivu na chuki
Kinyongo, wivu na chuki huambatana pamoja kama mapacha. 1Samweli 18:6 – 9 hapa tunaona Mfalme Sauli baada ya kusikia wanawake wakiimba na kumpa Daudi Makumi elfu nay eye maelfu moyo wake ulijaa kinyongo, wivu na chuki.
Matokeo yake ni mtu kuchukua uamuzi wa kulipa kisasi hata kama hujafanyiwa kosa, kwa sababu hii ndiyo tabia ya kinyongo, wivu na chuki. Na kama akishindwa kulipa kisasi aidha kwa sababu ya kuzidiwa nguvu au uwezo na yule aliyetaka kumlipiza kisasi, basi huchukua hatua ya kujizuru yeye mwenyewe akiona kama ndiyo njia ya kumaliza tatizo. 1Thesa 5:10 – 15, Math 2:16.
Hapo mtu afanyapo hivyo hajafanikiwa na kuponywa Kibiblia (Kimungu). Math 27:3 – 5. Hapo tunajifunza habari za Yuda mmoja wa wanafunzi wa Yesu, alivyogundoa tayari katenda kosa na kuamua
9
kurudisha vile vipande 30 vya fedha, lakini alipokosa uwezo wa kumfikia aliyemkosea alichukua uamuzi wa kujinyonga, ambao baadhi ya watu huutumia wakidhani wanatatua tatizo kumbe wanaongeza tatizo zaidi hadi kizazi chake chote. Mithali 17:13 “yeye arudishaye mabaya badala ya mema, mabaya hayataondoka nyumbani mwake”.
ii. Kukosa mahusiano mazuri na Mungu na kutofanikiwa katika jamii.
Tunaposoma habari za Adamu na Mkewe walipoanguka (kukosa) hawakutaka kuomba msamaha (kutubu) kama ilivyokuwa kwa Yuda, bali walianza kulaumiana na kufarakana. Mwanzo 3:12 – 13 katika jambo hilo mahusiano yao na Bwana Mungu yakawa mabaya yakutofanikiwa roho, nafsi na mwili kwani hapo ndipo ulipokuwa mwanzo wa hivi vitatu kutengana (roho, nafsi na mwili) kwani ilitokea hali ya kufa.
Leo watu wengi hawako tayari kukiri na kutubu kile walichokifanya ili waponywe na kufanikiwa, bali huwa 1. Wabishi 2. Wanaotaka ushahidi 3. Waliojaa malaumu 4. Wanaojitetea. Yoshua 7:16 – 22.
Hali hii humpelekea mtu kuwa na mahusiano mabaya na Mungu kwa jinsi roho, nafsi na mwili. Tunajifunza kuwa hali hii ilipelekea afamilia ya Adam nayo kufarakana kwa kupitia mkondo huo wa kutotaka kutubu, hebu ona mfarakano wa Kaini na Habil, Yakobo na Esau,
10
Isaka na Ishmaeli, Yusufu na nduguze. lakini pia mahusiano yao na Mungu yakawa mabaya. Mwanzo 4:6 – 8.
Hii yote ni kutokana na kinyongo, wivu na chuki binafsi juu ya mwenzio na tabia hii imeendelea mpaka kizazi chetu leo na inaanza kupenya hata kwa watu wa Mungu nao.
iii. Hujiona yuko sahihi kwa kile akifanyacho japo sisahihi (kujihesabia haki).
Kwa walimwengu wa leo kutosamehe kwao ni kawaida bali kusamehe kwao siyo kawaida, ndiyo maana dunia kila mahali pamejaa vita vya Taifa kwa Taifa, jamii kwa jamii au familia kwa familia yote hii ni hali ya kulipa kisasi na kutosamehe na kutoachilia. Mithali 24:6 – 7, Galatia 6:1 – 3.
Tunaona Biblia inatuhimiza kuwarudisha watu (mtu) ambaye amekosewa na kufikia kiwango cha kutokuwa rohoni, kwa hiyo unayejua sheria ya Kristo kama ipasavyo mrejeshe kwa kumshauri katika upendo. Zaburi 119:165 “wana Amani nyingi waipendao sheria yako. Wala hawana la kuwakwaza”.
iv. Huzuia mtiririko wa Baraka za Rohoni
Hali hii ikiruhusiwa na mtu bila kuchukua hatua za kuiondoa (kusamehe) husababisha kuziba njia kuu ya kutiririsha Baraka za Rohoni ambazo huja kwa njia ya Roho Mtakatifu, kwa kuwa mtu huwa
11
mchafu rohoni na hivyo Roho Mtakatifu hawezi kukaa mahali pachafu hata siku moja.
Mfano: Ikiwa wewe umepewa nyumba ya kuishi kwa nje imepambwa sana, lakini ndani kuna kinyesi, na mwenye nyumba hataki kukuruhusu ukitoe hicho kinyesi, sidhani kama unaweza kukaa humo, kwa sababu ya harufu mbaya. Na hivyo ndivyo ilivyo kwa Roho Mtakatifu na ndivyo alivyo mtu ambaye hana tabia ya kusamehe na kuachilia.
Msamaha hufungulia Baraka na mlango wa mafanikio yote.
1Petro 3:8 – 9 “Neno la mwisho ni hili, mwe na nia moja wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu wasikitivu, wanyenyekevu, watu wasiolipa baya kwa baya au laumu kwa laumu, bali wenye kubariki, kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi Baraka”.
Mungu wetu anapenda aone mambo mawili ya msingi kwetu ili atuponye na kutufanikisha.
A. Aone ndani moyo wa kusamehe na kuachilia
B. Aone ndani moyo wa kuomba msamaha.
Mithali 6:14 – 15, Marko 11:25 – 26 “Nanyi kila msimamapo na kusali sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu, ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makossa yenu, lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba aliye mbinguni hatawasemehe ninyi makossa yenu”.
12
Kumbuka
Tuliposikia Neno la Kristo, tuliamini na kukubali Bwana Yesu aingie moyoni mwetu kwa njia ya Imani, tukatubu kwa kuomba msamaha na Mungu akatusamehe, tukahesabiwa haki, hibyo mahusiano yetu yakawa mazuri mbele za Mungu. Maandiko hapo juu yanatufundisha kuwa tusamehe ili tusamehewe pia kwani kipimo kilekile tupimacho ndicho tutakachopimiwa, pia yanazama sana ndani kuwa kabla hatujafanya tendo la kuomba, kufanya Ibada kwa Mungu tuanze kusamehe waliotukosea.
Kwa kuwa bila kuomba Mungu, bila kufanya Ibada, bila kumtolea Mungu sadaka hakuna Baraka za Rohoni na mwilini lakini kabla ya yote kwanza tunaagizwa kusamehe na kuomba msamaha.
Math 5:23- 24.

MUNGU AKUBARIKI KWA VIWANGO VYA JUU!!!
LIMEANDALIWA NA MWL. MUSA FESTO
KWA MAWASILIANO NA USHAURI
NO: +255675415262
EMAIL:mussafesto@gmail.com.

Comments

Popular posts from this blog

JIFUNZE KUTII UPATE KUTIISHA