Posts

Showing posts from February, 2020

SIRI YA UPONYAJI

SOMO: SIRI YA KUPONYWA UTANGULIZI Tunaposema juu ya uponyaji na kufanikiwa haina maana juu ya uponyaji wa aina moja tu, yaani uponyaji wa mwili tu. Biblia inaposema uponyaji ina maana katika maeneo matatu yaani; 1. Uponyaji wa Rohoni 2. Uponyaji wa Nafsi 3. Uponyaji wa Mwili 3 Yohana 1:1 – 2 “Mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli. Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo” Efeso 1:3 “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa Baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo”. Zaburi 103:3 – 5 “Akusamehe maovu yako yote, akuponya magonjwa yako yote, aukomboa uhai wako na kaburi, akutia taji ya fadhili na rehema, aushibisha mema uzee wako, ujana wako ukarejezwa kama tai” 2 Petro 3:17 “Basi, wapenzi mkitangulia kujua hayo, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuucha uthabiti wenu”. 2 Katika maandiko hayo uaona kuna maeneo matatu yahusuyo up...

NGUVU YA MAAMUZI

SOMO: NGUVU YA MAAMUZI MAANDIKO 2 WAFALME 7:3 – 15, MITHALI 23:7a UTANGULIZI MAAMUZI NI NINI? MAAMUZI “ni chaguo analofanya mtu baada ya kufikilia jambo flani kulifanikisha" Majadiriano/kusemezana kwa mtu aidha na nafsi yake ama watu wawili tofauti juu ya jambo fulani lenye utata ndicho mama/kiini wa Maamuzi, lakini Maamuzi ni matokeo ya ndani ya mawazo ya mtu/watu au Jawabu la mawazo ya mtu/watu. 2 FALME 7:3 “Basi walikuwepo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji wakasemezana, mbona tunakaa hapa mpaka tufe? Tatizo moja kubwa sana ambalo huwa linachangia watu wengi wasiweze kufanikiwa katika maisha yao. Tatizo hili linaitwa kwa jina la hali ya KUSHINDWA/KUWA NA HOFU YA KUFANYA MAAMUZI KATIKA MAISHA. Kwa sababu ya kushindwa kufanya maamuzi watu wengi sana (hasa waliokoka/jamii ya waaminio) wamejikuta wakiwa katika hali zilezile bila kupiga hatua kwa muda mrefu sana katika maisha yao. Ukweli ni kuwa hali yako uliyonayo leo ni matokeo ya maamuzi ambayo uliyafanya huko ny...

SOMO: KUTOKA

SOMO: KUTOKA UTANGULIZI Kutoka ni kuhama kutoka nafasi ya chini au kutokuwepo mazingira ya kwanza kwenda mbele. Mfano unaweza kwenda kwa mtu au kwa rafiki yako usipomkuta utaamua kuulizia aliko watu watakujibu unayemtafuta hayupo katoka, maana yake mazingira hayo hayupo. Nilipokuwa ninasoma habari za wana wa Israeli walipokuwa wako utumwani Misri Mungu baada ya kuwaona wanateseka sana kwa kutumikishwa na Wamisri aliandaa mpango wa kuwatoa Nchi ya Misri ili kuwapeleka Nchi ya ahadi. Si rahisi kuelewa hali hii lakini pia mtumishi wa Mungu IBRAHIM Mungu alipotaka kumuinua na kumbariki awe taifa kubwa ambacho Mungu alikifanya ni kumwambia atoke katika Nchi ya baba yake na jamaa yake ili aende mahali atakapo ambiwa na Mungu, hiyo haitoshi baada ya Yesu kuja Duniani kwa mpango wa kumwokoa mwanadamu aliwakuta kina Petro wakivua samaki alichokifanya ni kuwatoa kwenye uvuvi wa samaki kuwaandaa ili wawe wavuvi wa watu. Swali je kwa nini Yesu asingewapa maagizo ya kuhubiri mpaka awatoe mahali wal...
ROHO MTAKATIFU NA KAZI ZAKE. Roho mtakatifu ni nani? 01.Roho mtakatifu ni nafsi halisi ya tatu ya Mungu baba. 02.Roho mtakatifu ni Mungu wa kweli. Lazima watu wote wajue ya kwamba Roho mtakatifu ni Mungu wa kweli aliye hai tena halisi. “ Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu. “ Matendo 5:3-4.  Angalia pia hapa “ Basi `Bwana’ ndiye Roho. ..”  2 Wokorintho 3:17 na Yoh.4:24 Kwa kuwa Roho ni Mungu wa kweli,basi hatunabudi kumuhitaji sana kwenye maisha yetu ya kila siku,tukamuishie Yeye tu kila siku. Yeye ndio kila kitu kwetu. Kitu ambacho hawakukitambua akina Anania na mkewe Safira kwamba Roho mtakatifu ni Mungu wa kweli,walifikiri ni mwanadamu tu hat...
MJUE MTUME PAULO Mtume Paulo ( 7 - 67 hivi) ni mmisionari mkuu wa Yesu Kristo katika historia ya Kanisa . Alitangaza kifo na ufufuko wake katika nchi karibu zote zilizopo kaskazini kwa Bahari ya Kati . Alimaliza ushuhuda wake kwa Yesu kwa kufia dini yake mjini Roma wakati wa dhuluma iliyoanzishwa na Kaisari Nero. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu . Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 29 Juni pamoja na ya Mtume Petro   Mtakatifu Paulo alizaliwa kati ya miaka 7- 10 BK katika familia ya Kiyahudi ya kabila la Benyamini (Israeli) na madhehebu ya Mafarisayo iliyoishi katika mji wa Tarsus (kwa sasa mji huo uko sehemu ya kusini mashariki ya nchi ya Uturuki ). Jina lake la kwanza (la Kiebrania ) lilikuwa Sauli , lakini kadiri ya desturi ya wakati ule alikuwa pia na jina la Kigiriki : Paulos kutoka Kilatini Paulus (= mdogo). Mwenyewe alikuwa na uraia wa Roma kama wananchi wote wa Tarsus. Angali kijana alisomea ualimu wa Sheria (y...
HISTORIA YA MAISHA YA MITUME 12 WA YESU Maisha ya Mitume/ wanafunzi wa kristo na wajibu waliopewa na Yesu kristo baada ya kristo kuondoka. Lengo hasa ni kutuwezesha kujua namna ambavyo waliotutangulia katika wokovu walivyokutana na changamoto ili na sisi tupige mbio zaidi katika kuutangaza ufalme wa Mungu. Hii ni kwa kuwa tumepokea hiki kijiti toka kwao hivyo na sisi tunayo safari yetu katika kristo YESU. Habari kuhusu Maisha ya Mitume hao na namna walivyosambaa duniani kote mpaka vifo vyao zinapatikana katika vitabu vilivyoandikwa katika kanisa la Kwanza. Schumacher ni Mwanahistoria wa kanisa aliyefanya utafiti kuhusu maisha ya mitume (wanafunzi wa kristo) na hivi ni namna ambavyo mitume hao walivyokumbana na misukosuko katika kumtangaza Kristo Yesu. 1. MATHAYO Huyu alikuwa mkusanya kodi (mtoza ushuru) kabla ya kumfuata Yesu. Mathayo ndiye alieandika kitabu cha Mathayo Mtakatifu. Alihubiri na kusambaza neno la Mungu huko Persia na Ethiopia ya sasa. Aliuawa kwa u...

JIFUNZE KUTII UPATE KUTIISHA

SOMO: UTII JIFUNZE KUTII UTIISHE Mwanzo 1:27 – 28 Maana ya neno UTII ni nini? UTII ni kukubali kitu kile ulichoagizwa kufanya na kukifanya; a) Kwa mwenendo mzuri na moyo safi b) Kwa wakati sahihi na mahali sahihi c) Na wakati mwingine bila kusimamiwa Isaya 1:18 – 19; Wafilipi 2:12 Kinyume cha neno utii ni KUASI : - Yaani kutenda kinyume na ulivyoagizwa au kutetenda kabisa(kugoma/mgomo). 1 Sam 15:17 – 23; 1 Yoh 3:4 Neno UTII lina kuja au kutokea baada ya kuwepo kwa neno agizo au amri. Maagizo au amri vinapotokea na utii ukachukua nafasi yake ya kutekeleza amri au maagizo, mambo haya yatatokea kwa aliyetoa agizo na aliyetekeleza agizo:-\ a) Ukamilifu b) Furaha c) Amani d) Upendo e) Upendeleo (kipaumbele) Mdo 10:34; Warumi 2:11 ; Mith 12:2 “ Mtu mwema atapata upendeleo kwa Bwan, bali mtu mwenye hila atahukumiwa naye. Mithali 13:15, 14:9, 35. Upendeleo huleta rehema tofauti ya hukumu iliyokwisha tolewa na itakayotolewa. Isaya 60:10;...