JIFUNZE KUTII UPATE KUTIISHA



SOMO: UTII
JIFUNZE KUTII UTIISHE
Mwanzo 1:27 – 28
Maana ya neno UTII ni nini?

UTII ni kukubali kitu kile ulichoagizwa kufanya na kukifanya;
a) Kwa mwenendo mzuri na moyo safi
b) Kwa wakati sahihi na mahali sahihi
c) Na wakati mwingine bila kusimamiwa

Isaya 1:18 – 19; Wafilipi 2:12
Kinyume cha neno utii ni KUASI: - Yaani kutenda kinyume na ulivyoagizwa au kutetenda kabisa(kugoma/mgomo).

1 Sam 15:17 – 23; 1 Yoh 3:4
Neno UTII lina kuja au kutokea baada ya kuwepo kwa neno agizo au amri.
Maagizo au amri vinapotokea na utii ukachukua nafasi yake ya kutekeleza amri au maagizo, mambo haya yatatokea kwa aliyetoa agizo na aliyetekeleza agizo:-\
a) Ukamilifu
b) Furaha
c) Amani


d) Upendo
e) Upendeleo (kipaumbele)

Mdo 10:34; Warumi 2:11; Mith 12:2 “Mtu mwema atapata upendeleo kwa Bwan, bali mtu mwenye hila atahukumiwa naye. Mithali 13:15, 14:9, 35.
Upendeleo huleta rehema tofauti ya hukumu iliyokwisha tolewa na itakayotolewa.
Isaya 60:10; Mith 29:26
Maana ya neno REHEMA

Rehema ni zaidi ya msamaha, kwani msamaha unatolewa pale mtu anapokosea na kuomba msamaha juu ya kile alichokosea, lakini rehema, mtu au Mungu humsamehe mtu hata bila kuomba msamaha, hiyo ndiyo rehema.
Kutoka 33:19; Kumb 5:10; Math 5:7; Yuda 1:21.
Maana ya neno KUTIISHA

KUTIISHA ni kumiliki eneo na vitu vilivyomo ndani yake. Mungu alipomuumba mwanadamu/mtu alimpa kumiliki Nchi na vilivyomo ndani yake, kama vile
i. Wanyama - Mwanzo 2:18 – 20;
ii. Samaki na ndege wa angani Mwanzo 1:26 – 31; Luka 5:1 – 8; Mathayo 17:24 – 27.
iii. Mimea
iv. Shetani, mapepo na magonjwa – Mwanzo 1:26 – 28 ; Marko 16:17; Luka 9:1 “Akawaita wale Thenashara(wanafunzi) akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi

Mungu alipompa mtu nafasi ya kumiliki dunia alimfanya kuwa mungu wa dunia.
Zaburi 82:6 “Mimi nimesema, ndinyi miungu na wana wa aliye juu, yote pia;
Zaburi 8:4 – 8 “Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu, umemvika taji ya utukufu na heshima, umemtawaza juu ya kazi za mikono yako, umevitia vitu vyote chini ya miguu yake……,
Zaburi 115:16; Yoh 10:34 – 35.
 Ni kwa jinsi gani Mtu alivyopoteza nafasi ya kumiliki na kutawala dunia:-
i. Ni kwa KUTOKUTII maagizo ya Mungu baada ya kudanganywa na shetani.

Mwanzo 3:1 – 19; 1 Yoh 3:4
Hivyo shetani alipofaulu kumtoa mtu katika maagizo ya Mungu na mtu kupoteza utii, nafasi ya kutawala dunia ilihamia kwa shetani akawa mungu wa dunia hii.
2 Kor 4:4 “Ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake kristo aliye sura yake Mungu ;
Luka 4:3 – 6; Waefeso 2:1 – 2; Yoh 12:31, 14:30.

Jinsi mwanadamu alivyopata tena nafasi ya kutawala( kuwa na mamlaka)
i. Nafasi hiyo mwanadamu aliipata tena baada ya ukombozi ulioahidiwa na Mungu katika bustani ya Edeni.

Mwanzo 3:14 – 15; Warumi 16:20; Math 1:18 – 20.
Ukombozi huu ulipatikana baada ya kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo pale msalabani, kwa kila mwanadamu anayemwamini anapewa uwezo wa kutawala yaani mamlaka ya kutawala vitu vilivyomo duniani (kutawala uumbaji wa Mungu).
a) Mapepo
b) Magonjwa
c) Na chochote ambacho kinaweza kuwa kikwazo katika maisha ya mtu aliyeokoka.

Math 28:16 – 19; Luka 10:17 – 20; Luka 9:1 – 6.
Pamoja na kauli hii ya neno la Mungu juu ya kuwapa mamlaka waumini lazima tufahamu kuwa siyo wote wanasema wameokoka, wanauwezo wa kutiisha au kuwa na mamlaka na amri juu ya vitu kama:
Mapepo, magonjwa, pamoja na vikwazo vingine.
Hii haijalishi kwamba ni Mchungaji, Mwinjilisti, Mwalimu, Askofu, Mtume, Nabii au Mlokole
Ila ni wale tu walio na uwezo wa KUTII neno la Mungu.
Marko 16:14 – 18 “……watashika nyoka, hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa, wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.
Pia siyo wote wenye funguo za kufunga na kufungua yale wanayoyataka au wasiyoyataka katika masiha yao.
Math 16:17 – 20
KUNA MAENEO MANNE TUNAPASWA KUTII KWAYO
1. Kutii NENO la Mungu
2. Utii katika uongozi wa kiroho
3. Utii katika uongozi wa Kifamilia
4. Utii katika uongozi wa kiserikali (waajiri)

Tunapoishi kwa kutii katika maeneo hayo manne kuna vitu tutakuwanavyo maishani mwetu hakika.
a) Amani - Waebrania 12:14; Zaburi 119:165
b) Furaha – Wafilipi 4:4; Marko 9:49 – 50
c) Haki – Mathayo 5:19 - 20
d) Imani safi – Yakobo 2:14; Waebrania 11:1

1. KUTII NENO LA MUNGU.
Neno la Mungu ni maandiko Matakatifu yaliyovuviwa uwezo na Mungu wa kufanya kila jambo jema.
Kuvuviwa maana yake ni kufanya wa hai au kuwa hai, hivyo NENO la Mungu li hai.Waebrania 4:12 “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzingawanya nafsi na roho ………
Na haya Maandiko Matakatifu yalikuwa ni mawazo ya Mungu, hatimaye yakawa ni maneno ya Mungu yaliyo sikiwa na watu na wakaamriwa kuyaandika
2Timotheo 3:16; Ufunuo 1:9 - 19 “Basi uyaandike mambo hayo uliyoyaona na yale yatakayokuwa baada ya hayo; - ; 2 Petro 1:19 – 20
Mawazo ni nini? Ni maneno yaliyofichwa katika ufahamu.
Maneno ni nini? Ni mawazo yaliyovikwa sauti – Mathayo 15:19, Marko 7:21; Waebrania 4:12 – 13
Neno la Mungu ni sauti ya Mungu, hivyo unapolitii unaendelea kujiweka kwenye mamlaka yake na kuendelea kuwa na sura ya Mungu na mfano wa Mungu. Yakobo 4:7
Kuwa na mfano wa Mungu ni kuwa na tabia ya Kimungu, moja ya tabia ya Uungu ni kutawala na kutiisha. Mwanzo 1:27 – 28.
Kutotii Neno la Mungu ni kujiondoa kwenye mamraka ya Mungu.
Mwanzo 2:16; 3:1 – 24
Hata shetani alishindwa kutii akaondolewa mbinguni. Mungu ni kiongozi wetu mkuu, ila anatuongoza kwa njia ya Neno lake
Zaburi 119:105; Yohana 1:1 – 5.
Bila Neno la Mungu hatuwezi kwenda sawa sawa na mapenzi ya Mungu ndio maana Musa alipovunja mbao zilizokuwa zimeandikwa amri za Mungu kwa ajili ya kuwaongoza, Mungu alirudia kuandika tena.
Kutoka 32:15 – 19; 34:4
Zaburi 119:105 “Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwangaza wa njia yangu”.
NENO LA MUNGU LINAMUAGIZA NINI MTU ANAYETAKA KUBARIKIWA.
(ili ubarikiwe lazima utoe sadaka).
Luka 19:26, Kumb 1:26 – 28).
Kumbuka kuwa Mungu mwenyewe ndiye mwanzilishi wa sadaka, kwa kumtoa mwana wake wa pekee ili aufie ulimwengu na ulimwengu upate ukombozi na uzima. Yohana 3:16.
Mtu anayetaka kubarikiwa lazima atii neno la Mungu, kisha atoe sadaka zote kama neno la Mungu linavyosema yaani kwa uaminifu
ZIKO AINA TANO (5) ZA SADAKA ZINAZOWEZA KUKUINUA NA UKAITWA BARAKA AU MBARIKIWA
Mwanzo 12:1 - 4; 17:1 – 5, 15
i. Sadaka ya Malimbuko
ii. Sadaka ya Hiyari
iii. Sadaka ya Nadhiri
iv. Sadaka ya Zaka 1/10
v. Sadaka ya Shukrani

Comments

Popular posts from this blog