SOMO: MAOMBI YA KUFUNGA.

UTANGULIZI.

Maombi ni muhimu sana kwa Mkristo aliyeokoka kwani maombi ni SILAHA.Tutazame maombi ya kufunga katika vipengele vikuu vitano

1 Kwanini tunafunga    2 Siku za kufunga   3 Faida za maombi ya kufunga

4 Hasara za kutokufanga      5 Kuisikia sauti ya Mungu

1.     KWANINI TUNAFUNGA?

Tunafunga ili kuisikizisha sauti yetu juu, kwa maneno mengine tunafunga ili kusikiwa na Mungu zaidi. Tunafunga ili kufungua vifungo vya uovu ambavyo vimeshindikana kwa maombi ya kawaida. Tunafunga ili kujinyenyekeza kwa Mungu kupata nguvu na Neema. Tunafunga ili kupata majibu ya haraka kwa mambo magumu. Tunafunga pia kwasababu maombi ya kufunga ni maombi yanayomgusa Mungu na kuvuta uwepo na nguvu zake hasa katika huduma. Tufunga pia ili kupata nguvu ya kuungamanisha Imani zetu kwa Mungu.

Danieli 10:1-3. 1 Katika mwaka wa tatu wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, Danieli, ambaye jina lake aliitwa Belteshaza, alifunuliwa neno; na neno lile lilikuwa kweli; maana ni vita vikubwa; naye akalifahamu neno lile, akaelewa na maono hayo. 2 Katika siku zile mimi, Danielii, nalikuwa nikiomboleza muda wa majuma matatu kamili. 3 Sikula chakula kitamu, wala nyama wala, divai haikuingia kinywani mwangu, wala sikujipaka mafuta kabisa, hata majuma matatu kamili yalipotimia.

Katika Danieli 9: 2 Danieli baada ya kuvisoma vitabu alifahamu hesabu ya miaka ambayo Mungu alikuwa amemwambia nabii Yeremia kuhusu Taifa la Israeli kuutimiza ukiwa Wa miaka Sabini. Danieli 9:3. Ndipo nikamwelekezea Bwana uso wangu, ili kutaka kwa maombi,na dua,pamoja na kufunga na kuvaa nguo za magunia na majivu. Bila shaka miaka ya kutolewa kwa taifa hili utumwani ilishatimia na kupita lakini hakuna aliyeona wala kutia akili, bali watu waliendelea na uovu wao mpaka hapa Danieli anapokuja kupitipitia vitabu anagundua hili jambo ambalo Mungu alikuwa ameshalitamka, inawezekana wakati wako wa kutoka utumwani ulishafika muda mrefu na tayari umeshapitiliza lakini kwa kuwa hujajua njia za kutoka hapo kwa kuutafuta uso wa Mungu kwa kufunga na kuomba bado umeendelea kufungwa katika kifungo hicho, Yesu aliwaambia wanafunzi wake katika Marko 9:29; Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lolote,isipokuwa kuomba, Ingia katika maombi ya kufunga ili kufungua na kuvunja hiyo nira,kama tulivyojifuza kazi ya maombi haya ya kufunga ni kuleta majibu ya haraka kwa mambo magumu,pia kuifanya sauti yako kusikiwa na Mungu na kupeleka Msaada wake wa haraka kwa mambo magumu, Esta, anaiingia katika Maombi ya siku tatu, yeye pamoja na vijakazi wake pamoja na Israeli wote, ili apate kibali kwa mfalme kinyume cha sheria, na Mungu alipeleka Msaada Wa haraka kupitia maombi ya kufunga akapata kibali kwa mfalme badala ya kuuwawa, mfalme akamnyoshea fimbo yake ishara ya kumkubali, Maana kama ingetokea mfalme asingemnyoshea fimbo yake basi kwa sheria za Mfalme AhasueroEsta angeuwawa kwani aliingia kinyume cha utaratibu. Esta 4:11, Watumwa wote Wa Mfalme, wanajua sana, hata na watu Wa majumba ya mfalme, ya kwamba mtu yoyote, akiwa mwanaume au mwanamke atakeyemjia mfalme katia uwa Wa ndani, wala hakuitwa kuna sheria moja kwake nayo ni kwamba auawe. Maombi ya kufunga yana uwezo Wa kukupenyeza mahali ambapo kwa hali ya kawaida usingepenya, yana uwezo wa kukuketisha na watu au mahali pa juu, mahali ambapo kwa elimu yako usingestahahili kuketi.

KIPENGELE CHA 2

SIKU ZA KUFUNGA: Ziko aina mbali mbali za kufunga Ila Mimi nitazungumzia aina kumi.

a.     Aina yetu ya kwanza ni kufunga kwa kuvusha mlo mmoja kwa mtu aliyezoea kula Milo mitatu kwa siku anatakiwa kuacha kula mlo mmoja.

b.     Funga ya pili,kuvusha milo miwili saa 24 ,unaacha kula asubuhi na mchana unakula jioni hii ndio funga ambayo watu wengi huependelea kufunga.

c.      Kuvusha Milo mitatu yaani moja, kavu saa 24.

d.     Kuvusha Milo sita yaani mbili kavu saa 48.

e.     Kuvusha Milo 9,tatu kavu masaa 72,,,,,,,,,,,,, ,=",-,: ,(,, ,, ,, 0);",Hii ndio funga aliyoifanya Esta, Esta 4:16 Uende ukawakusanye wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwaajili yangu,msile wala kunywa,muda wa siku tatu,usiku na mchana,nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile,kisha nitaingia kwa mfalme,kinyume cha sheria,nami nikiangamia na niangamie.

f.       Funga ya Danieli, kutokula vyakula vitamu, ,;Danieli alifunga kwa kula mtama na maji ,;Alifunga muda Wa majuma matatu, siku 21.

Danieli 10:2-3 Katika siku zile, Mimi Danieli nilikua nikiomboleza muda Wa majuma matatu kamili, Sikula chakula kitamu, wala nyama wala divai haikuigia kinywani mwangu, wala sikujipaka mafuta kabisa hata majuma matatu kamili yalipotimia.

g.     Funga ya Yohana Mbatizaji, Alifunga kwa kula chakula cha aina moja tu nzige na asali.

h.     Funga ya kulazimishwa hii ilimtokea Yona. Hapa Ni Mungu mwenyewe huhusika kumfungisha mtu/watu kwa kusudi lake mwenyewe Yona 1:17 Kisha Mungu akaamuru samaki mkubwa ammeze Yona,naye akawa tumboni mwa Samaki huyo kwa muda Wa siku tatu,usiku na mchana. Pia katika Matendo 27:33. Karibu na alfajiri,Paulo aliwahimiza,wote wale chakula" Kwa siku kumi na nne sasa mmekuwa katika Mashaka na bila kula,hamjala kitu chochote. Kuna watu ni waoga kufunga, wakati mwingine Mungu hutumia njia mbadala kama ya Yona na kina Paulo ili kuwafundisha kufunga.

i.       Funga ya Musa na YESU ya  siku 40

j.       Funga ya Hadhara au Taifa zima au kanisa zima. Mfano wa funga hii Ni wakati wa Corona Raisi wetu John Pombe Magufuli alitakaza maombi ya kufunga ya Taifa kwa muda wa siku tatu ili Mungu alinusuru taifa Letu na janga la Corona. Lazima funga ziwe siri na zifungwe kwa unyenyekevu mkubwa, unapofunga mtu yoyote asijue isipokuwa wewe na Mungu, labda iwe ni funga ya hadhara tena kama ni kanisa basi iwe siri kwa kanisa husika hata kanisa jingine lisifahamu, hii ni kwa sababu Biblia inasema katika Mathayo Sura ya,;6:16 Tena mfungapo msiwe kama wanafiki,wenye uso wa kukunjamana,maana hujiumbua nyuso zao,ili waonekane na watu kuwa wanafunga,Amini nawaambia wamekisha kupata thawabu yao, Bali wewe ufungapo jipake mafuta kichwani,unawe uso,ili usionekane na watu kuwa unafunga,Ila na Baba yako aliye sirini,na Baba yako aonae sirini atakujazi. Lazima funga ifungwe kwa furaha ya Roho Mtakatifu na sio kulazimishwa. Lazima funga iambatane na maombi. Tafuta muda mzuri Wa kuwa na utulivu na Mungu. Funga inakuwa na nguvu mtu anapoomba la sivyo unakuwa umekaa na njaa bure na kuuchosha mwili tu. Lazima funga iambatane na Upendo na sio ubinafsi, Hakikisha unapofunga unawapa wengine chakula chako, ambacho ungekula mchana. Isaya 58:6 Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira,kuwacha huru walionewa,kuwagawia wenye njaa chakula chako na kuwaleta masikini waliotupwa nje nyumbani kwako,Umwonapo mtu aliye uchi,umvike nguo,wala usijifiche na mtu mweye Damu moja nawe. Uko tayari kuingia kwa mfalme kinyume cha sheria kudai haki yako?

Basi chukua hatua ya maombi ya kufunga.

 

KIPENGELE CHA 3 FAIDA ZA KUFUNGA. Isaya 58:8-11…     8 Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde,

9 Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu; 10 na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri, 11 Naye Bwana atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.

Faida ya kwanza kulegeza kamba za nira. kama kuna vifungo vigumu vinafunguliwa. Nuru yako itapambazuka kama asubuhi, ukifunga wakati dunia inatembea katika Giza wewe uyefunga nuru ya Mungu inapambazuka. Isaya 60:1 Ondoka, uangaze kwa kuwa nuru yako imekuja maana Giza litaifunika dunia,na Giza kuu litazifunika kabia za watu, Bali Bwana atakuzukia wewe na utukufu wake utaonekana kwako.

Utapata haki zako bila kupigania, hutatafuta haki itakufuata ulipo. Kiu yako itakua adhuhuri, Giza lililokiwa kwako litakuwa nuru.

Utaponywa afya yako na mifupa yako itatiwa nguvu.

Funga huleta uponyaji. Bwana atakuwa kiongozi wako daima, utukufu Wa Mungu utakutangulia mbele ukulinde. Mungu ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji.

Mungu atakufanya uitwe heri. Utukufu Wa Mungu utakufuata nyuma ukulinde daima.

 

KIPENGELE CHA 4. HASARA ZA KUTOKUFUNGA

1.     kuna baadhi ya mambo hatawezekana Kwenye maisha yetu ya Kiroho. Mathayo 17:21 [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]

2.     Kazi ya Mungu itakuwa ngumu bila kuwa na maombi ya kufunga. Ndiyo maana Yesu aliye kielelezo chetu kabla ya kuanza kazi yake aliyotumwa na Mungu alianza kwa kufunga na kuomba.

3.     Nguvu za Kiroho zinakuwa kidogo na wakati wa Majaribu ujapo moyo huzimia Na kushindwa kustahimili. Mithali 24:10 Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache.

4.     Na tunapata nguvu za Mungu au nguvu za Kiroho kupitia maombi ya kufunga na kuomba.

5.     Huduma haitakua, utadumaa Kiroho,

6.     Mwili utaishinda roho. Maombi ya kufunga huutaabisha mwili na kuuthibiti ili utulie roho iyafanyayo mapenzi ya Mungu ipate kutawala. Marko 14:38 Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni, roho i radhi ila mwili ni dhaifu.

7.     Bila maombi ya kufunga kazi ya Mungu itafanyika kwa ulegevu na kuifanya kazi Mungu kwa ulegevu mwisho huleta laana katika maisha yetu kwa ujumla. Yeremia 48:10 Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya BWANA kwa ulegevu; na alaaniwe auzuiaye upanga wake usimwage damu.

 

KIPENGELE CHA 5. KUISIKIA SAUTI YA MUNGU.

Maombi ya kufunga hutuweka karibu sana na Mungu wetu na hutufanya kuisikia sauti ya Mungu wetu kwa kila jambo atuagizalo au anapotoa majibu yetu na hufanya tumwone Mungu.

Mfano Danieli baada ya kufunga na kuomba siku 21 sauti ya Mungu ilisikika kwake kwa ujumbe wa malaika. Danieli 10:2 Katika siku zile mimi, Danieli, nalikuwa nikiomboleza muda wa majuma matatu kamili. 3 Sikula chakula kitamu, wala nyama wala ,ai haikuingia kinywani mwangu, wala sikujipaka mafuta kabisa, hata majuma matatu kamili yalipotimia. 4 Na siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kwanza, nilipokuwa kando ya ule mto mkubwa, Hidekeli; 5 naliinua macho yangu, nikatazama, na kumbe, mtu aliyevikwa nguo za kitani, viuno vyake vimefungwa dhahabu safi ya Ufazi; 6 mwili wake pia ulikuwa kama zabarajadi safi, na uso wake mfano wa umeme, na macho yake kama taa za moto, na mikono yake na miguu yake rangi yake kama shaba iliyosuguliwa sana, na sauti ya maneno yake kama sauti ya umati wa watu. 7 Nami, Danieli, nikaona maono haya peke yangu; maana wale watu waliokuwa pamoja nami hawakuyaona maono haya; lakini tetemeko kuu liliwashika, hata wakakimbia ili kujificha. 8 Basi nikaachwa peke yangu, nikaona maono haya makubwa, wala hazikubaki nguvu ndani yangu; maana uzuri wangu uligeuzwa ndani yangu kuwa uharibifu, wala sikusaziwa nguvu. 9 Walakini naliisikia sauti ya maneno yake; nami niliposikia sauti ya maneno yake, ndipo nikashikwa na usingizi mzito, na uso wangu umeielekea nchi.

Maombi ya kufunga huushinda mwili na kuufisha na kufanya masikio yetu ya ndani kusikia mwito wa Mungu na macho yetu ya Kiroho kutiwa nuru.

Wagalatia 5:17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Waefeso 1:18 macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo.

Mungu akubariki kwa viwango vya juu!!.

Mwl. Musa Festo

Contacts: mussafesto@gmail.com

+255675415262.

#SalsalaPenyeMaziwanaAsali

 

Comments

Popular posts from this blog

JIFUNZE KUTII UPATE KUTIISHA