SOMO: UWAKILI

ANDIKO LA MSINGI 1 WAKORITHO 4:1.

Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu

 

UTANGULIZI.

Wakili ni nani: Ni msimamizi wa kazi au shughuli za mtu mwingine, ni mtetezi na mwangalizi.
Pia Wakili ni mwakilishi

Kwa hiyo Uwakili Ni kitendo cha mtu kusimamia kazi au shughuli za mtu mwingine na kuwa mwangalizi wa mtu mwingine, Pia ni kutekeleza jambo au kazi kwa niaba ya mtu mwingine
Huo ndio Uwakili

Kwa neno lingine naweza Sema Uwakilishi

 

Kazi za wakili

· Kumtambulisha yule anaye muwakilisha. (Tumevaa sura ya Kristo…Math. 26:73).

·        Kuhakikisha shughuli aliyopewa kusimamia inaenda jinsi alivyopanga Yule anayemwakilisha. Yesu anaweka wazi juu ya hali pale anapamwambia Baba yake(Mungu) juu ya kazi aliyomtuma duniani yaani kumwakilisha Mungu duniani na kumtukuza.(Yohana 17:4).

·        Kuwa mtetezi wa yule anaye mwakilisha

·        Kufanya kazi kama ambavyo angefanya mwakilishi wake. N.k

Wakili hawezi kufulahi kuona shughuli ya Bwana wake inadharauliwa na haifanikiwi katika kiwango kusudiwa bali Atatumia bidii yake kuhakikisha inaenda vizuri....

Wakili huwa ana act kama Bwana wake. Anafanya yale yote ambayo Bwana wake angeyafanya Tena Kwa ustadi mkubwa

Huyo Ndiye Wakili mwema anayejua kazi yake.

Nimekupitisha huko ili uone jinsi Wakili alivyo lakini leo nataka tumzungumzie Wakili wa Kristo.


Wakili wa Kristo ni nani?

Kila aliyemwamini Kristo na kumpokea anafanyika kuwa Wakili wa Kristo .Hivyo wewe uliyeokoka ni Wakili wa Kristo Na umefanyika kuwa shahidi wa Kristo Duniani

Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. Matendo ya Mitume 1:8

Uliyemkristo unafanyika kuwa shahidi (Wakili) wa Mungu katika ulimwengu. Umepewa kusimamia Kazi au shughuli na Mali za Mungu Unatakiwa kuushudia uhalisia wa Mungu Kwa Mataifa yote.

Sasa shida ipo hapo kwenye kuuishi Uwakili wetu. Shetani ametuvuruga na kutuingizia mambo Mengine mengi ambayo hayafanani na yule tunayemuwakilisha wala hayatoki kwake na tumeacha kufanya yaliyotupasa kuyafanya.

Yapo mengi shetani aliyoyahalalisha kwetu tuyaone kuwa ni Sawa Kumbe si Sawa balada ya kumwakilisha Mungu tunamdhalilisha Mungu wetu.

Wakili wa Mungu anapaswa kufanya yale mambo ambayo Mungu anataka kuyafanya Duniani
Kwa hiyo anafanya Kwa niaba ya Mungu( Mungu ni Roho hawezi kushuka duniani na kuihubiri injili na kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi wake ila ametupa sisi tulio milki yake kazi hiyo hapa duniani kama Mawakili wake yaani tunatenda kazi kwa niaba yake). Kama mawakili tunapaswa kupitisha Mapenzi ya Mungu Duniani ufalme wa Mungu ujulikane Duniani kupitia sisi.

Kwa mfano tumeuona Upendo wa Mungu juu ya watu wake hadi anamtoa wanawe wa pekee afe Kwa ajili ya watu wake

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Yohana 3 :16

Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Yohana 3 :17

Kwa hiyo ni kazi ya Wakili kuuendeleza Upendo ambao Mungu ameuanzisha Duniani. Maana Yesu anasema yeye ndiye njia kweli na uzima hivyo yatupasa kupita katika yeye tena anasema twaeni nira yangu mkajifunze kwangu…….. Sasa cha kushangaza Sisi tulio mawakili badala ya kudumisha Upendo Sisi tunazidi kuupoteza

Pia Tunaona lengo la Mungu kumtoa mwanawe wa pekee ni ili ulimwengu uokolewe
Kwa hiyo ni kazi ya Wakili kuhakisha wanadamu hawapotei bali wanaokolewa kama vile Mungu alivyo kusudia.


Hebu tuone jinsi Wakili wa Mungu anapaswa kufanya

1.     Wakili napaswa kumjua Mungu na kuzitambua siri za Mungu.

1 Kor 4:1.Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu

Kwanza kabisa ili uwe wakili wa Mtu Fulani ni lazima na muhimu kumfahamu vyema mtu huyo unayemtetea na kujua undani wake na jambo husika. Ni jambo la ajabu sana kumtumia Wakili katika kesi asiyejua sheria vizuri na vifungu vya sheria na hajui undani wa kesi yako, ni wazi kabisa hataweza kukutetea na mwisho utashindwa katika kesi yako hata kama uwezekano wa kushinda ulikuwepo.

Na sisi kwa sababu tu Mawakili wa Mungu tena Mawakili wa siri za Mungu ni lazima tumjue Mungu kwa undani sana na kuzitambua vyema siri za Mungu.

Tuwezaje kumjua Mungu na siri zake?

·        Kupitia Neno lake.  Tunamjua Mungu kupitia Neno lake kwani maandiko yanasema amejifunua kupitia Neno lake. Ndiyo maana Mandiko yanasema katika Wakolosai 3:16 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.

·        Tunaweza zijua siri za Mungu Kupitia Roho wake (Roho Mtakatifu).

Ili kuzijua siri za Mungu kama Mawakili wa Mungu lazima ndani yetu tuwe na Roho Mtakatifu kwani huyu ndiye pekee afunuae hata mafumbo ya Mungu na kutujulisha maana ni Mungu halisi. 1 Wakoritho 2:10 “Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu”.

Huyo Roho akiwa ndani yetu Utumishi wetu na Uwakili wetu wa siri za Mungu unakamilika nasi tunakamilishwa naye na kufikia utu uzima wa kufikia kima cha kumlingana Kristo YESU.

 

2.     Kumtambilisha Mungu Kwa Mataifa

Wakili wa Mungu ni kitambulisho cha Mungu. Kwa maana hiyo popote atakapo ingia wajue kuwa Mungu yupo mahali hapo. Ni lazima Wakili afanane na Mungu katika Utendaji, Watu wamuone Mungu ndani yake katika matendo (life style) yake yote yawe na utambulisho wa Mungu. Watu waamini kuwa Mungu Yupo na anatenda kazi kupitia Yeye.

3.     Kuhakikisha shughuli aliyopewa kusimamia unafanyika vile ilivyokusudiwa

angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda. Yeremia 1:10

Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. Mathayo 28 :19-20

Hiyo Ndio Kazi kubwa tuliyopewa Mawakili Kwa hiyo Wakili lazima ahakikishe hayo yote yanatukia jinsi ilivyokusudiwa. Ndiyo maana mtume Paulo anasema katika 1 Kor 4:1. Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.  Maandiiko yanaweka wazi lazima Wakili awe mwaminifu.

 

4.     Kuutete Ufalme wa Mungu. Wakili anapaswa kusimamia na kuutea ufalme wa Mungu na kutokukubari kuona ufalme wa Mungu unadhalilishwa na kuonekana si kitu Duniani
Bali Wakili atasimama na kuhakikisha ufalme wa Mungu unajulikana

5.     Kufanya Kazi Kama Ambavyo Mungu anataka ifanyike au Kufanya yale Mungu aliyoyakusudia Duniani.

Yesu alikuwa na huruma aliwahurumia Mataifa akawapa chakula, akawaponya, akawafufua
In short alifanyika msaada Kwa watu alikuwa utatuzi Kwa matatizo ya watu N.k
Hivyo Wakili anapaswa kuyadumisha hayo yote kama Mungu alivyokusudia.

 

 

HITIMISHO

Kanisa lililo mwili wa Kristo ni Wakili wa Kristo hivyo linapaswa kuyaishi maisha hayo na Mengineyo ambayo Mungu amelikusudia Kanisa liyaishi na liwe kimbilio la watu. Watu wakimwitaji Mungu wakimbilie kanisani wakutane na Mungu na kutatuliwa shida zao. Sasa Ebu tujiulize je Kanisa la leo linayaishi maisha hayo katika kiwango kusudiwa?

Wewe uliye Mkristo na kuhani - yaani mpatanishi wa watu na Mungu kwani Kuhani maana yake ni Mpatanishi wa watu na Mungu kama alivyo Kristo Je unayaishi maisha hayo?

Kama ndiyo Mungu na azidi kukupa Neema hiyo na kukubariki kwa viwango vya juu na kama siyo basi anza upya fufua uamsho ndani yako na kurudi katika nafasi yako ya                                                                       UWAKILI.

 

MUNGU AKUBARIKI KWA VIWANGO VYA JUU.

 

Mwl. Musa Festo

Contacts: mussafesto@gmail.com

+255675415262.

#SalasalaPenyeMaziwanaAsali

Comments

Popular posts from this blog

JIFUNZE KUTII UPATE KUTIISHA